MWADUI FC ya Shinyanga imeibuka bingwa wa michuano ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya timu za Ligi Kuu, kufuatia ushindi wa bao 1-0 jioni ya leo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Bao pekee la Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’, limefungwa na Salum Iyee dakika ya 85 akimalizia pasi maridadi ya kiungo Maregesi Mwangwa.
Mwadui imemaliza na pointi sita baada ya awali kuifunga na Toto African pia 1-0. Toto imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tatu baada ya kuifunga Kagera Sugar 2-0.
Stand United ya Shinyanga iliondolewa kwenye mashindano baada ya mechi moja tu na Mwadui ikifungwa 4-0, kufuatia kuchezesha wachzaji wa timu ya vijana, jambo ambalo lilikuwa kinyume cha kanuni.
Matokeo ya Stand United na Mwadui yalifutwa na michuano ikabaki na timu tatu- hatimaye leo Mwadui wameibuka mabingwa.

Kikosi cha Mwadui FC kilichoanza leo na kuibuka bingwa wa mashindano |
Stand United ya Shinyanga iliondolewa kwenye mashindano baada ya mechi moja tu na Mwadui ikifungwa 4-0, kufuatia kuchezesha wachzaji wa timu ya vijana, jambo ambalo lilikuwa kinyume cha kanuni.
Matokeo ya Stand United na Mwadui yalifutwa na michuano ikabaki na timu tatu- hatimaye leo Mwadui wameibuka mabingwa.
0 comments:
Post a Comment