// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MKWASA AWATUNUKU SIMBA SC ‘NISHANI’ YA UZALENDO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MKWASA AWATUNUKU SIMBA SC ‘NISHANI’ YA UZALENDO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, August 14, 2015

    MKWASA AWATUNUKU SIMBA SC ‘NISHANI’ YA UZALENDO

    Na Samira Said, DAR ES SALAAM 
    KOCHA mkuu w timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa, ameipongeza klabu ya Simba kwa maamuzi yao ya kuwaruhusu nyota wake kujiunga na kambi ya timu hiyo iliyomalizika leo jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo mjini Dar es Salaam, Mkwasa amesema kwamba kilichofanywa na Simba ni mfano wa kuigwa na wamekuwa wazalendo kwa nchi yao.
    Mkwasa alisema kuwa lengo la kambi yake ilikuwa ni kuangalia viwango vya wachezaji baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Kagame na wengine ambao hawakushiriki michuano hiyo kujua maendeleo yao.
    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (kushoto) amewapongeza Simba SC kwa uzalendo

    " Simba wamefanya vizuri sana na hii ndio inatakiwa kufanywa na wote kwa maslahi ya nchi,hata mazoezi yao ya asubuhi tumezingatia mechi yao ya kesho dhidi ya URA", alisema Mkwasa.
    Aliongeza kwamba bado anazishangaa Yanga na Azam kukataa kuwaruhusu nyota wake kujiunga na kambi hiyo yenye faida kuliko kwenda kucheza mechi za 'ndondo' Mbeya na Zanzibar ambako wameenda kuweka kambi.
    Aliongeza kuwa, kwa kufanya hivyo, Azam na Yanga imewakosesha nafasi wachezaji wake kutokana na benchi la ufundi kuita nyota wapya watakaosafiri kuelekea Uturuki katika kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.
    "Timu sasa inajengwa, hivyo tuliwaita ili tufanye mazoezi ya pamoja kabla ya kuelekea nje, ni nafasi ya vipaji vipya kuonekana", alisema kocha huyo.
    Taifa Stars inajiandaa na safari ya Uturuki kwa lengo la kujiimarisha kuikabili Nigeria katika mchezo utakaofanyika Septemba 5 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA AWATUNUKU SIMBA SC ‘NISHANI’ YA UZALENDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top