MSHAMBULIAJI Lionel Messi usiku huu amenusurika kadi nyekundu baada ya kumkwida na kumpiga kichwa Mapou Yanga-Mbiwa wakati Barcelona ikishinda 3-0 dhidi ya AS Roma katika mchezo wa kirafiki usiku wa Jumatano.
Roma wakiwa wamepagawa kwa kufungwa bao la mapema dakika ya 27 na Neymar Uwanja wa Nou Camp, nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Mapou akajikuta 'anamzingua' mvaa jezi namba 10 wa Barcelona kwa kuanza kumuonyesha ubabe.
Messi akajibu kwa kumpiga kichwa beki huyo Mfaransa kabla ya kumkwida shingoni. Refa Mspanyola, Javier Estrada Fernandez angeweza kuwatoa wote kwa kadi nyekundu- Mapou kwa kuanza ugomvia na Messi kwa kulipa kisasi, lakini akawaonya kwa kadi ya njano tu.
Mabao mengine ya Barca yalifungwa na Messi dakika ya 41 na Ivan Rakitic dakika ya 66.
Lionel Messi akizinguana na Yanga-Mbiwa kabla ya wawili wote hao kuonyeshwa kadi nyekundu Uwanja wa Nou Camp PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment