TIMU ya Manchester United imeanza vyema mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuichapa mabao 3-1 Bruges ya Ubelgiji usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford.
Kiungo wa United, Michael Carrick alianza kujifunga dakika ya nane kuwapatia wageni bao la kuongoza, kabla ya mchezaji mpya Memphis Depay kuwasawazishia Mashetani Wekundu dakika ya 13 na kuifungia la pili dakika ya 43.
Bruges ikapata pigo baada ya mchezaji wake, Brandon Mechele kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Kiungo aliyetokea benchi, Marouane Fellaini akaifungia bao la tatu United dakika ya 90- na sasa timu ya Louis Van Gaal itakwenda katika mchezo wa ugenini kulazimisha sare au kutofungwa zaidi ya 1-0 ili isonge mbele.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa; Romero, Darmian, Smalling, Blind, Shaw, Carrick/Schweinsteiger dk46, Schneiderlin, Mata, Januzaj/Hernandez dk72, Depay na Rooney/Fellaini dk83.
Club Bruges; Bruzzese, Cools, Mechele, Duarte, De Bock, Simons/Claudemir dk49, Vormer, Vazquez/Vanaken dk77, Bolingoli Mbombo, Dierckx na Diaby/Oulare dk56.
Memphis Depay akishangilia baada ya kuifungia Manchester United mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Bruges jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment