MBABE Floyd Mayweather amesema kwamba atapigana na Andre Berto katika pambano lake la 49 Septemba 12, mwaka huu.
Pambano hilo litafanyika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena, Mayweather akipanda ulingoni akiwa hajawahi kupoteza hata pambano moja kuelekea pambano lake la 50.
Mara ya mwisho Mayweather kupanda ulingoni alimshinda kwa pointi za majaji wote, Mfilipino Manny Pacquiao Mei mwaka huu akishinda kwa mara ya 48 mfululizo.
Floyd Mayweather ametaja pambano lake la 49 kwamba atapigana na Andre Berto Septemba 12 mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment