// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MASHUJAA BAND IPO HAJA YA KUANZA UPYA …SIMAMISHENI MAONYESHO MUINGIE KAMBINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MASHUJAA BAND IPO HAJA YA KUANZA UPYA …SIMAMISHENI MAONYESHO MUINGIE KAMBINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, August 17, 2015

    MASHUJAA BAND IPO HAJA YA KUANZA UPYA …SIMAMISHENI MAONYESHO MUINGIE KAMBINI

    KATIKA moja ya bendi za dansi za kizazi kipya ambazo zina tungo nzuri na muziki ulioshiba ipasavyo basi Mashujaa Band ni moja wapo.
    Lakini Mashujaa imekuwa ni moja ya bendi inayobadilika rangi mara kwa mara jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linawachelewesha kufika kwenye kilele cha mafanikio  …Mashujaa iliyokuwa chini ya Elyston Angai, Kadjo na Chaz Baba ni vitu vitatu tofauti na kati ya hatua zote hizo hakuna hata moja iliyofanikiwa kutimiza njozi zake.
    Wakati hatua moja ikionekana kuanza kushika kasi basi litataokea jambo litakalozalisha mabadiliko ya kiongozi wa bendi na kisha safari kuanza upya.
    Elyston Angai amerejea tena Mashujaa Band hali inayotoa picha kuwa bendi hiyo inangia kwenye rangi nyingine kwa mara nyingine tena.
    Unapohudhuria maonyesho ya Mashujaa Band kwa wiki za hivi karibuni hususan pale Mashujaa Lounge wanapopiga kila Ijumaa na Jumapili utabaini kuwa hali ya mahudhurio ya mashabiki si nzuri.
    Mashujaa ni bendi iliyojizolea mafanikio ya haraka haraka ikiwemo kutwaa jumla ya tuzo 9 za Kilimanjaro Tanzania Music Awards ndani ya miaka mitatu – mara ya kwanza ilitwaa tuzo tano, mwaka uliofuta tuzo tatu na mwaka huu imechukua tuzo moja.
    Lakini licha ya mafanikio hayo ya kimuziki, licha ya kuwa na wanamuziki mahiri, Mashujaa Band bado haikuwa na mafanikio ya kujivunia kwenye kumbi za starehe hususan jijini Dar es Salaam ambako sehemu kubwa ya mwaka jana tuliishuhudia ikipiga kwa kiingilio cha ‘kinywaji chako’.
    Ni wazi kuwa Mashujaa Band inahitaji kujipanga upya ili kufikia kule inakostahili kufika bendi yenye nyenzo na menejimenti bora kama Mashujaa – bendi inayomilikiwa na kampuni yenye kumiliki kumbi mbili za starehe, kituo kimoja cha radio, biashara ya usafiri na vikorombwezo kibao.
    Je Elyston Angai ni suluhisho? Ni suala linahohitaji subira …hakuna ubishi kuwa Elyston ni mwanamuziki mahiri lakini ubora wake kwa hapa Tanzania unapimwa zaidi na mafanikio aliyoyazoa ndani ya muda mfupi kwenye bendi ya Diamond Sound iliyotambwa mwishoni mwa miaka ya 90.
    Ungeweza kumpima pia Elyston Angai kupitia bendi ya Vibration Sound chini ya Aset lakini kwa bahati mbaya alishindwana na waajiri wake kabla bendi hajaichanganya na hatimaye kuuzwa kwa kampuni ya Mashujaa.
    Hata ndani ya Mashujaa Band, Elyston pia hakudumu kwa muda mrefu, alitibuana na wamiliki wake na kuamua kujidumbukiza kwenye muziki wa kumtukuza Mungu na baadae kurejea Afrika Kusini yalipokuwa maskani yake kwa muda mrefu.
    Kwa mtazamo wangu, wanachotakiwa kufanya Mashujaa Band ni kusimamisha maonyesho ya bendi hasa yale ya Ijumaa na Jumapili kwenye ngome yao ya Mashujaa Lounge ambayo naamini kwasasa yanakwenda kwa hasara hivyo hawatakuwa na cha kupoteza.
    Kwanini wasimamishe maonyesho? Wasimamishe ili bendi iingie kambini na kutengeneza nyimbo bab kubwa, wapotee machoni mwa mashabiki wao ili wakiibuka wawe ni kitu kipya, waongeze angalau mwimbaji mmoja mpya ambaye akiungana na Diperon na rapa Mirinda Nyeusi ambao bao hawajasikika hewani kwenye kazi mpya za Mashujaa, basi ni wazi kuwa watafanya sura ya ushambuliaji ya bendi hiyo iwe muonekano mpya.
    Katika kipindi ambacho bendi itakuwa kambini, menejimenti ya Mashujaa ihakikishe kunakuwa na ‘fitna’ za kutosha kupitia vyombo vya habari juu ya kile kinachopikwa kambini …ndani ya kipindi hicho, Mashujaa Band iachie angalau nyimbo mbili mpya zenye mashiko, zifanyiwe kampeni kubwa kwenye vituo vya radio, mitandao ya kijamii, ikibidi na kwenye televisheni kabla ya kuandaa onyesho kubwa la kuitambulisha upya Mashujaa yenye rangi mpya, wasanii wapya na nyimbo mpya.
    Ninaamini kuwa iwapo Mashujaa Band watakuwa na nyimbo kali na mashabiki kuitika vilivyo kwenye onyesho la kwanza na kisha wanamuziki wake wakafanya makamuzi ya kufa mtu jukwaani, basi huo utakuwa ni mwanzo mzuri katika kuijenga Mashujaa mpya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHUJAA BAND IPO HAJA YA KUANZA UPYA …SIMAMISHENI MAONYESHO MUINGIE KAMBINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top