BONDIA Amir Khan amepewa nafasi ya kupigana na Manny Pacquiao Mashariki ya Kati, wakati Floyd Mayweather akiwa bado hayuko tayari kupigana naye.
Promota wa Pacquiao, Bob Arum ataanza mazungumzo na uongozi wa bondia huyo wa Bolton wiki hii kujadili juu ya pambano hilo baada ya kukataliwa na Mayweather.
Wakati bondia bora wa mwaka atapigana na Andre Berto mjini Las Vegas Septemba 12, pambano la Khan na Pacquiao, linaweza kufanyika mapema mwakani.
Mtendaji Mkuu wa The Top amependekeza pambano lifanyike Mashariki ya Kati badala ya Vegas, ingawa tayari amekataa kulipeleka Dubai.
"Huyu mtoto Amir Khan anazidi kuchonga kuhusu Manny Pacquiao. Naweza kuandaa pambano la Khan apigane na Pacquiao,"amesema Arum akizungumza na The Telegraph.
Pac-Man alilalamika kuumia bega lake kulia wakati anapoteza pambano kwa pointi mbele ya Mayweather Mei mwaka huu, lakini Arum amesema anaendelea vizuri na atakuwa tayari kurejea ulingoni mwaka 2016.
Pacquiao alishindwa kwa pointi na Mayweather katika pambano lake la mwisho mjini Las Vegas Mei mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment