// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED WAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, WAICHAPA 1-0 SPURS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED WAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, WAICHAPA 1-0 SPURS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 08, 2015

    MAN UNITED WAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, WAICHAPA 1-0 SPURS

    KOCHA Louis Van Gaal ameweka kibindoni pointi tatu katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur mchana wa leo Uwanja wa Old Trafford, Manchester.
    Shukrani kwake, beki wa Spurs, Kyle Walker aliyejiufnga dakika ya 21 na kuwapa mwanzo mzuri Mashetani Wekundu msimu wa 2015/2016.
    Winga mpya Memphis Depay alikuwa kivutio akicheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya England, wakati kiungo Bastian Schweinsteiger alitokea benchi kuchukua nafasi ya Michael Carrick.
    Kikosi cha Manchester United kilikuwa: Romero, Darmian/Valencia dk80, Smalling, Blind, Shaw, Schneiderlin, Carrick/Schweinsteiger dk60, Young, Mata, Rooney na Depay/Herrera dk67. 
    Tottenham Hotspur: Vorm, Walker, Alderweireld, Vertonghen, Davies, Dier/Alli dk76, Bentaleb/Mason dk52, Chadli, Eriksen, Dembele/Lamela dk69 na Kane.

    Nahodha Wayne Rooney akibinuka tik tak katika mchezo dhidi ya Spurs leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED WAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, WAICHAPA 1-0 SPURS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top