// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LILI NDIYE MSHINDI WA KINONDONI TALENT SEARCH 2015 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LILI NDIYE MSHINDI WA KINONDONI TALENT SEARCH 2015 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, August 17, 2015

    LILI NDIYE MSHINDI WA KINONDONI TALENT SEARCH 2015

    Na Somoe Ng'itu, DAR ES SALAAM
    LILIAN Michael ameibuka mshindi katika shindano la kusaka wasanii wenye vipaji katika Wilaya ya Kinondoni (Kinondoni Talent Search 2015) lililofanyika usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam.
    Kutokana na ushindi huo, Lilian amezawadiwa kitita cha Sh. Milioni tano na kulipiwa gharama za kurekodi vibao atakavyoandaa kwa muda wa mwaka mmoja na Ofisi ya Utamaduni ya Wilaya ya Kinondoni.
    Lillian Michael kushoto akiwa na Mpoki 

    Mshindi huyo kwa mara ya kwanza alipoanda jukwaani aliimba wimbo uitwao Njiwa ambao uliwahi kuimbwa na mkongwe wa taarabu, Patricia Hilary, kwa ufasaha na kumfanya Mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuimba pia na kuucheza.
    Shindano hilo lililoingiza washiriki 15 katika hatua ya fainali, pia lilimpata mshindi wa kucheza, Raidanus Vitalis, ambaye naye alipata zawadi iliyofanana na Lilian.
    Nurdin Bakari 'Baloteli' yeye aliibuka mshindi katika upande wa kuchekesha ambapo karata yake iliyomuingiza kwenye hatua ya mwisho ilikuwa ni jinsi gani mtoto wa Rais anavyopata tabu kupata 'makopo' ya kuchezea wakiwa Ikulu ndipo baba alipomueleza mkewe kuchukua hata katiba ya nchi ampe mtoto achezee kauli iliyowavunja mbavu wageni waliohudhuria akiwamo Rais Kikwete.
    Msanii huyo alilia kwa furaha kutokana na kuibuka mshindi na kuweka wazi kwamba amepitia mazingira magumu katika kazi yake hiyo na kueleza yeye ni mchekeshaji wa mitaani lakini akampongeza Mpoki kwa kumsaidia kumuonyesha njia ya mafanikio ambayo imeanza kuonekana kupitia shindano hilo.
    Mwasisi wa shindano hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, alisema kwamba lengo la kuanzisha shindano ni kutoa nafasi kwa vijana kujipatia ajira kupitia vipaji walivyonavyo na kuongeza kwamba litafanyika kila mwaka.
    (Somoe Ng'itu ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LILI NDIYE MSHINDI WA KINONDONI TALENT SEARCH 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top