// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ‘LIGI KUU NDOGO’ KUPIGWA KAMBARAGE KUANZIA JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ‘LIGI KUU NDOGO’ KUPIGWA KAMBARAGE KUANZIA JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 04, 2015

    ‘LIGI KUU NDOGO’ KUPIGWA KAMBARAGE KUANZIA JUMAMOSI

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    CHAMA cha Soka Shinyanga (SHIREFA), kwa kushirikiana na kampuni ya Cleverland Res ya Mwanza, wameandaa mashindano maalum ya timu za Ligi Kuu za Kanda ya Ziwa Victoria.
    Mratibu wa mashindano hayo, Kabole Kahungwa ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba michuano hiyo itashirikisha timu zote za Kanda ya Ziwa zilizopo Ligi Kuu na yatafanyika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
    Amezitaja timu hizo kuwa ni Stand United, Mwadui FC zote za Shinyanga, Toto African ya Mwanza na Kagera Sugar ya Bukoba.
    Kikosi cha Stand United kilichoshiriki Ligi Kuu msimu uliopita

    Kahungwa, mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba SC ya Dar e Salaam amesema mashindano hayo ni maalum kwa ajili ya kuzipa maandalizi timu za Kanda ya Ziwa kabla ya Ligi Kuu.
    “Kama unavyoona timu za Kanda ya Ziwa zimefanya usajili mzuri kuelekea Ligi Kuu, kwa hivyo na sisi tukaona tuziandalie mashindano baina yao ili kujiweka fiti,”amesema Kahungwa.
    Ligi Kuu inatarajiwa kuanza wiki ya pili ya Septemba na Kanda ya Ziwa msimu huu itakuwa na nne, kutoka mbili za msimu uliopita Kagera Sugar na Stand United, baada ya kupanda kwa Toto na Mwadui.

    AGOSTI 8, 2015
    Stand United Vs Mwadui FC
    AGOSTI 9, 2015
    Toto African Vs Kagera Sugar
    AGOSTI 10, 2015
    Mwadui FC Vs Toto Africans
    AGOSTI 11, 2015
    Kagera Sugar Vs Stand United
    AGOSTI 12, 2015
    Stand United Vs Toto African
    AGOSTI 13, 2015
    Mwadui FC Vs Kagera Sugar
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘LIGI KUU NDOGO’ KUPIGWA KAMBARAGE KUANZIA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top