Angban wa pili kulia walioinama akiwa katika kikosi cha Simba SC jana |
Mabao ya Simba SC jana yamefungwa na Mussa Hassan Mgosi kipindi cha kwanza na Elius Maguli kipindi cha pili.
Angban aliyewahi kudakia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Chelsea ya England, alianzia Azam FC, lakini hakukubalika mbele ya kocha Muingereza Stewart Hall akaomba kujaribu bahati yake na Simba SC.
Na kocha Muingereza wa Simba SC, Dylan Kerr akamuanzisha jana katika mchezo wa kirafiki na kudaka vizuri, timu ikishinda kwa mara ya tatu mfululizo mechi za kirafiki visiwani humo.
Awali Simba SC iliifunga Kombaini ya Zanzibar 2-1 kabla ya kuifunga 4-0 Black Sailor hapo hapo Uwana wa Amaan na kesho watacheza na Jang’ombe Boys kabla ya Jumatano KMKM Saa 10:00 jioni.
Hamisi Kiiza akiwania mpira dhidi ya kipa wa Polisi |
Mussa Mgosi akipambana na beki wa Polisi |
0 comments:
Post a Comment