// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIMBEMBE LIGI KUU CHAANZA LEO, MAN UNITED NA TOTTENHAM, CHELSEA NA SWANSEA CITY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIMBEMBE LIGI KUU CHAANZA LEO, MAN UNITED NA TOTTENHAM, CHELSEA NA SWANSEA CITY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 08, 2015

    KIMBEMBE LIGI KUU CHAANZA LEO, MAN UNITED NA TOTTENHAM, CHELSEA NA SWANSEA CITY

    LIGI Kuu ya England inatarajiwa kuanza leo, mabingwa watetezi Chelsea wakifungua dimba na Swansea City Uwanja wa Stamford Bridge, London kuanzia Saa 1:30 usiku.
    Kikosi cha Jose Mourinho hakikuwa na amtokeo mazuri katika mechi za kujiandaa na msimu wakipoteza mechi tatu na leo kitajaribu kutafuta mwanzo mzuri wa kutetea taji.
    Manchester United watakuwa wenyeji wa Tottenham Hotspur Uwanja wa Old Trafford kuanzia Saa 8:45 mchana, wakati Norwich City wataikaribisha Crystal Palace Uwanja wa Carrow Road kuanzia Saa 11:00 jioni.
    Leicester City watakuwa wenyeji wa Sunderland Uwanja wa King Power Saa 11:00 jioni muda ambao pia Everton watamenyana na Watford Uwanja wa Goodison Park na Bournemouth na Aston Villa Uwanja wa Vitality.
    Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo kati ya 
    Newcastle United na Southampton Uwanja wa St. James' Park kuanzia Saa 9:30 Alasiri, muda ambao pia Arsenal watakuwa wanamenyana na West Ham United Uwanja wa Emirates, wakati Saa 12:00 jioni Liverpool watakuwa wageni wa Stoke City Uwanja wa Britannia.
    Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya England utakamilishwa keshokiutwa kwa mchezo kati ya mabingwa wa zamani, Manchester City dhidi ya West Bromwich Albion Uwanja wa The Hawthorns kuanzia Saa 4:00 usiku.

    RATIBA KAMILI MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND:
    Jumamosi Agosti 8, 2015
    Manchester United v Tottenham Hotspur (Old Trafford, Saa 7:45 mchana)
    Norwich City v Crystal Palace (Carrow Road, Saa 11:00 jioni)
    Leicester City v Sunderland (King Power, Saa 11:00 jioni)
    Everton v Watford (Goodison Park, Saa 11:00 jioni)
    Bournemouth v Aston Villa (Vitality,  Saa 11:00 jioni)
    Chelsea v Swansea City (Stamford Bridge, Saa 1:30 usiku)
    Jumapili Agosti 9, 2015
    Newcastle United v Southampton (St. James' Park, Saa 9:30 Alasiri)
    Arsenal v West Ham United (Emirates, Saa 9:30 Alasiri)
    Stoke City v Liverpool (Britannia, Saa 12:00 jioni)
    Jumatatu Agosti 10, 2015
    West Bromwich Albion v Manchester City (The Hawthorns, Saa 4:00 usiku)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIMBEMBE LIGI KUU CHAANZA LEO, MAN UNITED NA TOTTENHAM, CHELSEA NA SWANSEA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top