// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KCCA WASHINDI WA TATU KAGAME, WAITANDIKA 2-1 KHARTOUM N TAIFA, WAONDOKA MILIONI 20 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KCCA WASHINDI WA TATU KAGAME, WAITANDIKA 2-1 KHARTOUM N TAIFA, WAONDOKA MILIONI 20 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 02, 2015

    KCCA WASHINDI WA TATU KAGAME, WAITANDIKA 2-1 KHARTOUM N TAIFA, WAONDOKA MILIONI 20

    KCCA ya Uganda imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuifunga mabao 2-1 Khartoum N ya Sudan.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao ya KCCA yamefungwa na Muzamiru Mutyaba na Michael Birungi, wakati bao pekee la Khartoum N limefungwa na Osmaila Baba.
    Na kwa ushindi huo, KCCA itapata zawadi ya fedha, dola za Kimarekani 10,000 (Sh. Milioni 20 za Tanzania) wakati Khartoum inaondoka mikono mitupu sawa na timu nyingine zilizotolewa awali.
    Fainali ya michuano hiyo inafuatia Saa10:00 kati ya Gor Mahia ya Kenya na Azam FC ya Tanzania na bingwa ataaawadiwa dola 30,000 (Sh. Milioni 60) mshindi wa pili dola 20,000 (Sh. Milioni 40).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KCCA WASHINDI WA TATU KAGAME, WAITANDIKA 2-1 KHARTOUM N TAIFA, WAONDOKA MILIONI 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top