// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KATI YA YANGA SC YA TANZANIA NA REAL MADRID YA HISPANIA NANI ZAIDI? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KATI YA YANGA SC YA TANZANIA NA REAL MADRID YA HISPANIA NANI ZAIDI? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 09, 2015

    KATI YA YANGA SC YA TANZANIA NA REAL MADRID YA HISPANIA NANI ZAIDI?

    SEPTEMBA 1, mwaka 2014, Javier Hernandez Balcazar maarufu kwa jina la utani ‘Chicharito’ alisaini Real Madrid kwa mkopo wa muda mrefu msimu mmoja kutoka Manchester United.
    Alikwenda kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini siku hiyo hiyo kabla ya kukabidhiwa jezi namba 14 aliyokuwa anavaa Xabi Alonso kabla ya kuondoka.
    Na Septemba 13 akacheza mechi yake ya kwanza Real Madrid, akitokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya Karim Benzema dakika 27 za mwisho timu hiyo ikifungwa 2–1 na Atletico Madrid.
    Septemba 19, Hernandez akafunga mabao yake mawili ya kwanza Real Madrid baada ya kutokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya Gareth Bale dakika ya 77 katika ushindi wa 8–2 ugenini dhidi ya Deportivo de La Coruña.
    Akafunga bao la ushindi Aprili 22, mwaka huu dhidi ya Atletico Madrid, akiiwezesha Real Madrid kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Na Mei 26, mwaka huu, Hernandez akarejea nyumbani Manchester baada ya kumaliza muda wake wa kucheza kwa mkopo Santiago Bernabeu.
    Wakati Chicharito anaondoka Manchester timu hiyo ilikuwa iko vibaya, haifanyi vizuri- lakini Real Madrid walikuwa wapo vizuri na ndiyo walikuwa mabingwa wa Ulaya.
    Lakini kocha Carlo Ancelotti aliona anahitaji mshambuliaji mzuri wa akiba kwa wakati ule na akagundua Man United kuna mtu ni mzuri, lakini hana nafasi, akamuomba akapewa.
    Chicharito wakati anaondoka pale mbele Man United kuna Robin van Persie, Radamel Falcao, Wayne Rooney na Danny Welbeck ilikuwa bado haijakamilika kwenda Arsenal.
    Lakini sasa anarejea, hakuna Van Persie, Falcao wala Welbeck na usajili wa kocha Louis Van Gaal umegusa maeneo mengine zaidi, si washambuliaji wa kati hadi sasa.
    Wiki hii, Yanga SC iliwasilisha maombi Azam FC kuwaomba kwa mkopo wachezaji wawili, beki Bryson Raphael na kiungo Mudathir Yahya.
    Bahati mbaya, Azam FC wakasema hawawezi kumtoa Mudathir- labda Raphael, ambaye ni beki wa kulia.
    Siku zote nasema, Yanga SC safari hii wamepata Katibu Mkuu bora kabisa, mweledi na mbunifu- pia asiyependa klabu iwe na mahusiano mabaya na wadau wengine.
    Kitendo tu cha kuwaandikia Azam FC kuomba wachezaji kwa mkopo maana yake kinawadhihirishia kwamba Yanga haina tatizo nao na kama ni upinzani wa kugombea mataji ni wa uwanjani tu.       
    Ukiitazama Azam FC ilivyo Raphael na Mudathir ni wachezaji ambao Azam FC haiwezi kuwauza, lakini kwa sasa ni vigumu kwao kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Azam FC kulingana na nafasi zao kusheheni ‘mafundi’ na wazoefu.
    Kwa kuwa ni vijana wadogo, Azam FC ina mipango nao ya muda mrefu na hilo yule Katibu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha ameliona ndiyo maana akawaomba kwa mkopo Mudathir na Raphael kipindi hiki.
    Yanga SC nao ni kweli wanahitaji kiungo wa beki wa kushoto wa akiba- kwa kuongezea pia, Yanga SC wanahitaji pia mshambuliaji aina ya Malimi Busungu wa akiba.
    Huyo Mudathir ambaye kwa Azam FC anasubiri mbele ya akina Kipre Balou, Jean Baptiste Mugiraneza, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Himid Mao na sasa Ame Ally ‘Zungu’ naye anatumika kama kiungo, kwa Yanga SC anaweza akawa anapokezana na Haruna Niyonzima na Salum Telela. 
    Na kwa kuwa mahitaji ya Yanga SC ni kiungo aina ya Mudathir kwa nini klabu iingie gharama kusajili mchezaji mwingine wakati kuna uwezekano wa kumpata kwa mkopo kinda huyo wa Azam FC?
    Nani anadhani wakati Real Madrid inamchukua kwa mkopo Chicharito, ilikuwa haina uwezo wa kununua mshambuliaji sehemu nyingine popote?
    Wale wenzetu Wazungu, sisi huku kwa uswahili wetu kitendo cha Yanga kumuomba kwa mkopo Mudathir watu wamekwishaanza kukandia.
    Eti Yanga kuomba mchezaji kwa mkopo Azam FC ni kujishusha, basi kama ni hivyo Real Madrid klabu tajiri zaidi duniani kwa miaka ilijishusha zaidi kwa Manchester United kumchukua kwa mkopo Chicharito.
    Wakati umefika Watanzania tubadilike. Tuendeshe soka kama ambavyo wanaendesha wenzetu, ili nasi tufanikiwe kama wao.
    Zamani tulifanya mambo kienyeji kwa sababu hatukuwa kwenye dunia ya utandawazi, tulisubiri kusikiliza Idhaa za Kiswahili za BBC na Sauti ya Ujerumani, ili kujua dunia inavyoendelea, lakini hivi sasa tunaona kwa macho yetu kupitia Televisheni na tunasoma kwenye intaneti moja kwa moja. Ushamba bado wa nini?
    Najaribu kutafakati katika wale viongozi wa Yanga ninaowajua, Mwenyekiti Yussuf Manji, Clement Sanga, Isaac Chanji, Aaron Nyanda, Abdallah Bin Kleb, Seif Magari nani mshamba pale? Simuoni.
    Sasa kama hivyo ndivyo kwa nini Yanga SC mambo bado ya kizamani? Au tujiulize, Real Madird na Yanga SC nani zaidi? Alamsiki. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KATI YA YANGA SC YA TANZANIA NA REAL MADRID YA HISPANIA NANI ZAIDI? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top