// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HABARI NJEMA SIMBA SC, NDAYISENGA ANARUDI KUSAINI MSIMBAZI, WAKALA KADITO ALAINIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HABARI NJEMA SIMBA SC, NDAYISENGA ANARUDI KUSAINI MSIMBAZI, WAKALA KADITO ALAINIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, August 28, 2015

    HABARI NJEMA SIMBA SC, NDAYISENGA ANARUDI KUSAINI MSIMBAZI, WAKALA KADITO ALAINIKA

    Mshambuliaji Mrundi, Kevin Ndayisenga anarudi kusaini Simba SC baada ya klabu kumalizana na waka wake 

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imefikia makubaliano na wakala Dennis Kadito kuhusu mshambuliaji Mrundi, Kevin Ndayisenga na sasa mchezaji huyo anakuja kusaini timu ya Msimbazi.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba Ndayisenga anarudi kusaini baada ya kumalizana na wakala wake, Kadito.
    “Mazungumzo yetu ya awali na Kadito hayakufanikiwa kwa sababu kadha wa kadha. Lakini imekuwa bahati tumerudi mezani tena na tumefikia makubaliano, sasa Ndayisenga anarudi,”amesema Poppe, Kapteni wa zamani wa Jeshi lwa Wananchi Tanzania (JWTZ).
    Kuhusu washambuliaji wengie wawili wa majaribio, Makan Dembele wa Mali na Pape Abdoulaye N’daw wa Senegal, Poppe amesema atasajiliwa mmoja wao. “Na si lazima tusajili, tunaweza kuachana na wote iwapo hawataonyesha uwezo wa kuridhisha,”amesema.
    N’daw kesho atafanyiwa mtihani wa kwanza wa majaribio wakati Simba SC itakapomenyana na Mafunzo Uwanja wa Amaan, Zanzibar, wakati Dembele anatarajiwa kutua usiku huu.
    N’daw anatokea klabu ya Dinamo Bucuresti ya Ligi Kuu ya Romania wakati Dembele anatokea JS Kabyle ya Algeria.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HABARI NJEMA SIMBA SC, NDAYISENGA ANARUDI KUSAINI MSIMBAZI, WAKALA KADITO ALAINIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top