MABINGWA watetezi, Chelsea wamekiona cha moto kwa Manchester City baada ya kuchapwa mabao 3-0 usiku wa leo Uwanja wa Etihad katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Sergio Aguero alianza kuifungia Manchester City dakika ya 32 katika mchezo ambao mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa alidhibitiwa vikali wakati beki John Terry alitolewa na kocha Jose Mourinho kwa mara ya kwanza baada ya mechi 177.
Nahodha wa City, Vincent Kompany akafunga bao la pili dakika ya 79, kabla ya Fernandinho kufunga la tatu dakika ya 85.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Manchester City: Hart, Sagna, Mangala, Kompany, Kolarov, Toure, Fernandinho, Navas/Nasri dk65, Silva, Sterling/Demichelis dk79 na Aguero/Bony dk83.
Chelsea; Begovic, Ivanovic, Cahill, Terry/Zouma dk45, Azpilicueta, Ramires/Cuadrado dk64, Matic, Willian/Falcao dk79, Fabregas, Hazard na Diego Costa.
Sergio Aguero akimzidi Gary Cahill kuifungia City bao la kwanza PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment