Na Somoe Ng'itu, DAR ES SALAAM
MWAMUZI Msaidizi mwenye beji ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), Ferdinand Chacha, ndiye refa pekee Mtanzania ambaye ameteuliwa kuchezesha katika Michezo ya Afrika (All Africa Games) ambayo mwaka huu itafanyika Congo Brazaville.
Fainali hizo zinatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 4 hadi 19 kwa kushirikisha michezo mbalimbali huku kwa upande wa soka, timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) nayo imefuzu kushiriki mashindano hayo.
Akizungumza kwa simu kutoka Mwanza, Chacha (pichani chini), alisema kuwa anaamini amepata mafanikio hayo kutokana na umakini wake anapochezesha mechi mbalimbali za kimataifa anazopangiwa kuchezesha ndani na nje ya nchi.
Chacha alisema kwamba mazoezi binafsi anayofanya kila siku ndiyo yanamsaidia kulinda kiwango chake na yeye si refa anayesubiri kujinoa pale mtihani wa majaribio "Cooper Test" unapokaribia.
Alisema kuwa anaumia kuona katika mashindano makubwa ya soka, timu ya Tanzania (Taifa Stars) inatolewa mapema na Watanzania kubakia watazamaji wa mataifa mengine ya Afrika au Ulaya yakichuana.
Refa huyo alisema kwamba tangu aanze kuchezesha soka ni mwaka jana ndipo alikumbana na changamoto baada ya Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kubadilisha marefa wa mechi ya Simba na Yanga katika dakika za lala salama.
" Iliniumiza na ilinichanganya sana, mechi hiyo huwa na mambo mengi, siwezi kusahau kwa nini ilifanyika maamuzi mengine", alisema Chacha.
Refa huyo aliongeza kwamba bado Tanzania ina safari ndefu kuelekea katika mafanikio na hiyo inatokana na tatizo la miundombinu ambayo inawaathiri kuanzia waamuzi hadi klabu zetu za hapa nchini.
Chacha alianza kuchezesha soka rasmi mwaka 2002 akiwa ni mwamuzi wa Daraja la Nne huku Ligi Kuu alianza kuchezesha msimu wa mwaka 2007/ 2008 mchezo uliozikutanisha Mtibwa Sugar na Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na ilimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Aliutaja mchezo wake wa kwanza wa kimataifa kuchezesha akiwa na beji ya Fifa aliyoipata mwaka huo huo wa 2012 ilikuwa ni kati ya Congo Brazaville dhidi ya Club Sportive Faxien ya Tunisia huku mwamuzi wa kati alikuwa ni Waziri Shekha kutoka Zanzibar.
" Katika ukanda wa Cecafa tunaenda waamuzi wawili, mimi na mwenzangu kutoka Burundi anaitw Patrick, na tatizo la kukosekana kuitwa kwenye fainali kubwa ni kufeli mitihani ya mafunzo na utimamu wa mwili tunayofanya kila inapoandaliwa", Chacha alisema.
Mbali na kuwa ni mwamuzi, Chacha ni Mhasibu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na aliajiriwa serikalini tangu mwaka 2005 ikiwa ni miezi nane tangu ajiunge na Chuo cha Biashara cha CBE, Dar es Salaam ambapo alimaliza masomo yake 2008.
"Taaluma yangu inanisaidia sana ninapokuwa nje ya nchi kwenye mashindano, mwaka jana nilipokuwa Botswana kwenye mashindano ya vijana mkufunzi alishangaa na hapo hapo akaniambia nitakuwa kiongozi wa waamuzi", aliongeza.
Chacha alimaliza elimu ya Msingi mwaka 1993 katika Shule la Sabasaba mkoani Iringa na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari iitwayo Lugalo huku kidato cha tano na sita akisoma Shycom mkoani Shinyanga.
(Somoe Ng'itu ni Mwandishi wa gazeti la Nipashe)

0 comments:
Post a Comment