TIMU ya Athletic-Bilbao imefanikiwa kutwaa taji la Super Cup ya Hispania licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji Barcelona Uwanja wa Camp Nou usiku huu.
Sare hiyo ya ugenini, inafanya Athletic Bilbao ichukue Super Cup kwa ushindi wa jumla wa 5-1, baada ha wiki iliyopita kushinda 4-0 nyumbani.
Lionel Messi alianza kuifungia Barcelona dakika ya 43, kabla ya Aritz Aduriz kuisawazishia Bilbao dakika ya 75.
Gerard Pique wa Barca alitolewa kwa kadi nyekundu sawa na Kike Sola wa Bilbao mwishoni mwa mchezo.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Bravo, Pique, Rakitic/Munir dk68, Sergio, Alves, Pedro/Sandro dk68, Iniesta, Suarez, Messi, Mascherano na Mathieu.
Athletic Bilbao: Iraizoz; De Marcos, Balenziaga, Etxeita/Elustondo dk68, Laporte, Gurpegi, Benat/Mikel Rico dk83, Eraso, Boveda, Aduriz/Kike Sola dk81 na Susaeta.
Athletic Bilbao: Iraizoz; De Marcos, Balenziaga, Etxeita/Elustondo dk68, Laporte, Gurpegi, Benat/Mikel Rico dk83, Eraso, Boveda, Aduriz/Kike Sola dk81 na Susaeta.
Athletic Bilbao, washindi wa pili wa Kombe la Mfalme mwaka jana, wakisherehekea Super Cup ya Hispania baada ya kuifunga jumla ya mabao 5-1 Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment