BAO pekee Robert Lewandowski dakika ya 87, limeipa Bayern Munich ushindi wa 1-0 Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich Ujerumani dhidi ya Real Madrid na kutwaa Kombe la Audi, michuano maalum ya kujiandaa na msimu.
Pep Guardiola alikutana na Real Madrid 'dhaifu' kidogo ambayo haikuwatumia nyota wake kama Cristiano Ronaldo na Gareth Bale ambao wote walipumzishwa katika mchezo.
Mshambulaiji huyo wa kimataifa wa Poland alifunga bao hilo pekee akimalizia shuti la mpira wa adhabu uliopigwa na Douglas Costa mbele ya mashabiki 70,000 mjini Munich.
Wachezaji wa Bayern Munich wakisherehekea na Kombe la Audi usiku wa jumatano Uwanja wa Allianz Arena PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment