WENYEJI Bayern Munich wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AC Milan jana katika mchezo wa Kombe la Audi Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.
Kwa ushindi huo, Bayern Munich sasa itamenyana na Real Madrid katika fainali ya Kombe la Audi usiku wa leo, wakati AC Milan itawania nafasi ya tatu dhidi ya Tottenham iliyofungwa na Real 2-0.
Mabao ya Bayern Munich jana yalifungwa na Juan Bernat dakika ya 24, Mario Gotze dakika ya 73 na Robert Lewandowski zikiwa zimesalia dakika sita.
Kiungo mpya, Arturo Vidal aliyesajiliwa kutoka Juventus ya Italia jana aliichezea kwa mara ya kwanza Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena.
Kikosi cha Bayern Munich kilikuwa; Ulreich, Rafinha, Boateng, Lahm/Alonso dk56, Kimmich/Alaba dk19, Hojbjerg, Rode, Bernat, Vidal, Costa/Lewandowski dk46 na Gotze.
AC Milan; Lopez, De Sciglio, Zapata/Alex dk63, Ely, Antonelli, De Jong, Bertolacci, Bonaventura, Honda, Luiz Adriano na Bacca.
Arturo Vidal ameichezea kwa mara ya kwanza Bayern Munich jana ikishinda 3-0 Uwanja wa Allianz Arena PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment