TIMU ya Real Madrid ya Hispania imeifunga mabao 2-0 Tottenham Hotspur ya England katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Audi mjini Munich jana.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Allianz Arena jana, bao la kwanza la Real lilifungwa na James Rodriguez dakika ya 36 kabla ya Gareth Bale kuiadhibu timu yake ya zamani kwa kufunga bao la pili dakika ya 79.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casilla, Danilo, Varane, Ramos/Nacho dk68, Marcelo/Arbeloa dk59, James/Vazquez dk46, Modric/Illara dk59, Kroos/Casemiro dk46, Isco/Asensio dk68, Bale/Mayoral dk82 na Jese/Cherychev dk59.
Tottenham; Vorm, Walker, Alderweireld, Wimmer/Vertonghen dk46, Rose, Dier/Bentaleb dk46, Alli/Winks dk69, Lamela/Chadli dk46, Dembele, Eriksen/Carroll dk69 na Kane/Onomah dk86.
Gareth Bale akipambana na beki wa Tottenham, Eric Dier Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment