// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
AZAM TV WAZINDUA CHANELI MPYA YA MICHEZO TUPU ITAKAYOONYESHA LA LIGA NA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEAZAM TV WAZINDUA CHANELI MPYA YA MICHEZO TUPU ITAKAYOONYESHA LA LIGA NA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
AZAM TV WAZINDUA CHANELI MPYA YA MICHEZO TUPU ITAKAYOONYESHA LA LIGA NA LIGI KUU
KAMPUNI ya Azam Media leo imezindua rasmi chaneli yake mpya yenye ubora wa juu kabisa, iitwayo “Azam Sports HD”.Tangu kuanza kwa huduma za AzamTV, wateja wamekuwa wakijiuliza hasa ni kipi wanachopata kutokana na alama ya HD iliyo mbele ya kisimbuzi – kuanzia sasa watabaini. Baada ya miezi 18 ya mipango na uwekezaji, leo umeshuhudiwa uzinduzi wa chanel ya kwanza itakayowezesha wateja kufaidi picha na sauti zaubora wa juu kabisa “HD” kutokana na teknolojia ya kiwango cha juu.
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Tido Mhando akizungumza katika hafla hiyo
Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington akizungumza katika hafla hiyo
Waalikwa mbalimbali wakifuatilia zoezi hilo
Wateja wa kifurushi chenye chaneli mpya ya “Azam Sports” wataweza kuona timu zao wazipendazo katika VPL katika picha ang’avu zaidi ambazo hazijawahi kuonekana. Zaidi, kampuni pia imetangaza rasmi ujio wa Ligi Kuu ya Hispania maarufu La Liga ambayo wateja wataipata katika ubora wa HD kupitia Chanel mpya. Mchezo wa kwanza kuoneshwa katika msimu mpya wa La Liga 2015/16, ni Malaga dhidi ya Seville wa Ijumaa Agosti 21, 2015 na timu zote vigogo zitakuwa zikicheza na kuoneshwa Live mwisho wa juma lijalo, na kila mzunguko wa msimu mzima katika ubora wa HD.
Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam Media, Mgope Kiwanga akizungumza wakati wa hafla hiyo
Waalikwa mbalimbali wakati wa zoezi hilo leo
Maofisa wa Azam TV wakijadiliana mambo wakati wa shughuli hiyo
Kifurushi kinachojumuisha chaneli ya Azam Sports HD kitaonekana kwa watazamaji wa AzamTV wa Tanzania pekee ambao wanalipia kifurushi chochote kati ya vitatu vya sasa; Pure, Plus au Play – na nyongeza ya ya SH15,000 kwa mwezi, ikijumuisha VAT. Pamoja na chaneli mpya ya Azam Sports HD, malipo hayo yatajumujisha chaneli za klabu za Manchester United, Liverpool na Real Madrid ambazo kwa sasa ni sehemu ya kifurushi cha Azam Play. Kadhalika malipo ya mwezi kwa kifurushi cha Play kitapunguzwa hadi Tsh25,000 kuanzia sasa. Kwa wale wasiokuwa na luninga zenye uwezo wa kuona picha za HD au waya maalum wa HD (HDMI), watapata chaneli mpya na kufuatilia La Liga na mengineyo – japo si kwa ubora wa HD. Pia kwa wateja wasiohitaji kujiunga na kiufurushi kipya hawapaswi kuwa na wasiwasi wa kutoona michezo ya VPL kwani itaendelea kuoneshwa kupitia Azam One na Azam Two kama ilivyokuwa kabla – Jambo lililo tofauti ni kuwa michezo yenye mvuto zaidi itaoneshwa pia kwenye Azam Sports HD. Zaidi ya La Liga na VPL, Azam Sports HD itakuwa na vipindi mbalimbali vya kimichezo vitakavyojumuisha michezo ya Ligi za soka za Uganda, Kenya na, Burundi – itakayoanza hivi karibuni. Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amesema “Uzinduzi wa Azam Sports HD ni hatua kubwa katika maendeleo ya AzamTV.
Mwenyeki wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Muhammad alikuwepo
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Said Tuliy kulia na Collin Frisch kushoto
Hata kabla ya ya kuanza mwaka 2013 tulijipanga kukidhi mahitaji ya teknolojia kwa ajili ya kutoa picha za ubora wa HD ili kutuwezesha baadaye kumpatia mtazamaji picha bora zaidi bila kulazimika kununua vifaa vipya. Jambo ambalo hatukulitazamia ni kutekeleza hilo ndani ya muda mfupi – na kuanzisha chaneli kwa kuonesha moja kwa moja soka la La Liga! Ambalo ni bora zaidi barani Ulaya. Uwezo wa kuona moja kwa moja na katika HD timu mzipendazo huko Hispania na kwa VPL, pamoja na vipindi vingine vya michezo kutoka sehemu mablimbali duniani, unatoa chaguo muhimu na ambalo wateja wetu wanalimudu. Huu ni mwanzo tu – jiandae kwa makubwa zaidi”
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment