Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
AZAM FC imefuta mpango wa kumtoa kwa mkopo winga wake Mganda, Brian Majwega na pia imesema haina kabisa mpango wa kumuacha mshambuliaji wake Mrundi, Didier Kavumbangu.
Awali, Azam FC ilikubali kumrudisha Majwega KCCA FC kucheza kwa mkopo, baada ya kocha wake, Muingereza Stewart Hall kumtoa kwenye mipango yake ya msimu ujao.
Lakini akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kwamba mpango huo ulikuwapo awali, lakini kwa sasa umekufa.
“Ni kweli kulikuwa kuna mpango huo, lakini kwa sasa umekufa, anabaki katika timu,”amesema Kawemba.
Akizungumzia uvumi ulioenea mjini kwamba, Kavumbangu atapelekwa Simba SC kwa mkopo, Kawemba amesema; “Hakuna mpango kama huo, Kavumbangu ni mchezaji wa Azam FC na anaendelea kuutumikia Mkataba wake wa miaka miwili iliyobaki,” amesema.
Majwega hakuwamo kwenye orodha ya wachezaji 20 waliocheza Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Azam FC ikitwaa ubingwa wiki iliyopita na kocha Hall alisema ni kwa sabnabu alikuwa mgonjwa.

Azam FC imesema haina mpango wa kumtema Mrundi Didier kavumbangu |
“Ni kweli kulikuwa kuna mpango huo, lakini kwa sasa umekufa, anabaki katika timu,”amesema Kawemba.
Akizungumzia uvumi ulioenea mjini kwamba, Kavumbangu atapelekwa Simba SC kwa mkopo, Kawemba amesema; “Hakuna mpango kama huo, Kavumbangu ni mchezaji wa Azam FC na anaendelea kuutumikia Mkataba wake wa miaka miwili iliyobaki,” amesema.
Majwega hakuwamo kwenye orodha ya wachezaji 20 waliocheza Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Azam FC ikitwaa ubingwa wiki iliyopita na kocha Hall alisema ni kwa sabnabu alikuwa mgonjwa.
0 comments:
Post a Comment