// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAMTEMA MAJWEGA, ARUDISHWA KCCA KWA MKOPO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAMTEMA MAJWEGA, ARUDISHWA KCCA KWA MKOPO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 08, 2015

    AZAM FC YAMTEMA MAJWEGA, ARUDISHWA KCCA KWA MKOPO

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    WINGA Mganda Brian Majwega atarudishwa KCCA FC kucheza kwa mkopo, baada ya kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart Hall kumtoa kwenye mipango yake ya msimu ujao.
    Baada ya kusajiliwa kwa Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Simba SC na kupona kwa Farid Mussa na Joseph Kimwaga- winga Mganda Majwega amejikuta anapoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Azam FC.
    Majwega hakuwamo kwenye orodha ya wachezaji 20 waliocheza Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Azam FC ikitwaa ubingwa wiki iliyopita na tayari mipango ya kumpeleka kwa mkopo KCCA imeanza.
    Brian Majwega (kulia) amefunga bao moja tu Azam FC katika mechi 28 za msimu wake wa kwanza na sasa anarudishwa kwa mkopo KCCA FC ya kwao Uganda 

    Mtendaji Mkuu wa KCCA FC, David Tamale amekaririwa na 

    Kawowo Sports ya Uganda akisema kwamba; 

    “Ni kweli,” alisema baada ya kuulizwa juu ya mipango ya kumrejesha Majwega KCCA FC. “Tupo katika majadiliano ya mwisho na ni matumaini, itakuwa imekamilika kabla ya wiki ijayo,” amesema Tamale.

    Majwega alijiunga na Azam FC Desemba mwaka jana na hadi sasa ameichezea mechi 28 na kuifungia bao moja tu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAMTEMA MAJWEGA, ARUDISHWA KCCA KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top