MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC wameendeleza wimbi la ushindi katika mechi ya 13 mfululizo chini ya kocha Muingereza, Stewart Hall baada ya kuichapa JKU mabao 2-0 usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na Nahodha na mshambuliaji na Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 59, akimalizia pasi maridadi ya kiungo Mudathir Yahya Abbas na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 88 kwa shuti kali la mbali.
Azam FC imeweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 22 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Yanga SC.
Na huo ni mchezo wa tatu mfululizo timu hiyo ya Chamazi, Mbade, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kushinda katika kambi yao ya Unguja, baada ya awali kuzifunga KMKM 1-0 na Mafunzo 3-0.
Na kwa ujumla katika mechi zote 13 chini ya Stewart tangu arejee Juni mwaka huu, Azam FC imefungwa mabao mawili tu katika mechi ya kwanza kabisa dhidi ya Friends Rangers Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Baada ya hapo, nyavu za Azam FC hazijaguswa tena kuanzia kwenye mechi za kirafiki hadi Kombe la Kagame na hizi tatu za kirafiki Zanzibar- jumla mechi 12 makipa wa Azam FC ‘hawajalokota kunyavu’.
Na kwa ujumla katika mechi zote 13 hadi leo, Azam FC chini ya Hall, imefunga jumla ya mabao 24- maana yake ina ukuta mgumu na fowadi tishio kwa wapinzani.
Wapinzani wao katika mchezo wa Ngao, Yanga SC wapo kambini Tukuyu, Mbeya ambako jana wameshinda mechi ya tatu ya kujipima wakiilaza MBeya City 3-2 baada ya awali kuzifunga Kemondo 4-1 na Prisons 2-0.

0 comments:
Post a Comment