WAKATI Manchester United wakiwa Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya, mchezaji wao Angel Di Maria aliendelea kubaki nyumbani kwao Argentina bila idhini ya klabu yake.
Hata siku aliyoambiwa sasa ni lazima urejee kazini, bado mchezaji huyo akaendelea kuwa mtukutu na hakutokea kazini, kocha wake Louis van Gaal akasema ni lazima amkate mshahara wa wiki mbili.
Di Maria alikuwa kwenye mgomo baridi akishinikiza klabu yake imuuze kwenda PSG na mwisho wa siku utashi wake ukatimia, Manchetser United wakakubali kumpiga bei.
Mwimbaji mkongwe wa dansi la kizazi kipya Rogart Hegga wiki iliyopita alionekana akifanya mazoezi na Twanga Pepeta huku akiwa hajatokea kazini kwake (Mashujaa Band) kwa zaidi ya wiki tatu.
Rogart aliyetambulishwa Mashujaa Band kwa kishindo wiki chache kabla ya mapumziko ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, akakamatwa na uongozi wa Mashujaa na kupelekwa polisi, akawekwa kwa masaa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa masharti ya kurejesha pesa alizopewa na bendi hiyo kama ada ya ‘usajili’ wake, hiyo ikimaanisha kuwa ‘ndoa’ yake na Mashujaa Band imevunjika na yupo huru kujiunga na bendi nyingine.
Jumamosi usiku Rogart Hegga akapanda jukwaa la Twanga Pepeta na kushiriki onyesho maalum lililopewa jina la “Usiku wa Dream Team” lililofanyika Mango Garden Kinondoni.
Tunaambiwa Twanga Pepeta ilimuomba Rogart Hegga ashiriki onyesho hilo, lakini hata baada ya Rogart kukubali, bado Twanga haikutaka kujali kama Mashujaa imetoa Baraka zake au la, wao msimamo wa msanii waliyemtaka uliwatosha na wakaingiza jina lake kwenye matangazo ya kunadi onyesho hilo …hapa nahisi kama Twanga Pepeta hawakutenda haki.
Kwa hili Twanga Pepeta wanapaswa kuvaa kiatu cha Mashujaa ili waone uchungu wa msanii wao kutangazwa kwenye onyesho la bendi nyingine bila ridhaa yao tena huku na wao wakiwa na kazi katika siku hiyo hiyo.
Inawezekana kabisa kuwa Rogart Hegga alikuwa anafanya mgomo baridi kama wa Di Maria ili atimuliwe kazi na apate kurejea kirahisi bendi yake ya zamani, Lakini Twanga Pepeta walipaswa kukaa kando kwenye ‘mchezo’ huo hadi msanii huyo na Mashujaa watakapomalizana.
Chaz Baba - mwimbaji mwingine wa Mashujaa naye akaibuka kwenye onyesho hilo la Twanga Pepeta licha ya onyo la bendi yake kuwa ni marufuku msanii wa Mashujaa kushiriki onyesho hilo …hapa sina cha kuwalaumu Twanga Pepeta.
Tunajua wazi kuwa Twanga haikumtaja Chaz Baba hata sehemu moja kwenye matangazo ya onyesho hilo, hivyo msalaba wa utukutu huo unapaswa kubebwa na Chaz Baba mwenyewe, Twanga isingeweza kumkataza kupanda jukwaani maana wasanii kusalimiana kisanii ni jambo la kawaida.
Di Maria alifanya utukutu wa makusudi ili Manchester United wachukie na wamuuze na kweli ikawa hivyo, inawezekana kuwa hata Chaz Baba naye pia anatumia mbinu za Di Maria ili kuwakera ‘waajiri’ wake na waamue kumwagana nae …Mashujaa Band wanapswa kuwa makini sana kwenye matukio haya, wanaweza kabisa wakajikuta wanampiga chura teke wakidhani wanamkomoa kumbe wanamuongezea mwendo.
Bendi zetu zinabidi zijifunze kupitia somo hili la “Dream Team” ya Twanga Pepeta na matukio mengine kama haya yaliyopita huko nyuma - zihakikishe kuwa wanayoyatenda kwa wenzao basi na wao wawe tayari kutendewa.
Bendi zijifunze pia kusoma alama za nyakati juu ya wasanii wao, zifahamu historia na tabia za wasanii kabla hazijaamua kuwasajili, zitafakari kwa kina kama msanii wanayemtaka anakidhi vigezo na anaendana na mfumo wa bendi.
Wasanii nao wafahamu kuwa muziki ni kazi kama kazi nyingine hivyo wanaposaini mikataba au kuingia makubaliano ya aina yoyote ile, basi ni vema kuiheshimu kwasababu ni mkataba huo huo watakautegemea uwaokoe pale mwajiri atakapokwenda kinyume.

0 comments:
Post a Comment