ARSENAL imeanza vibaya msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 2-0 na West Ham United Uwanja wa Emirates jioni ya leo.
Cheikhou Kouyate alianza kufunga akitumia makosa ya kipa Petr Cech kuipatia West Ham bao la kwanza dakika ya 43, kabla ya Mauro Zarate kufunga la pili dakika ya 57.
Adrian aliokoa michomo kadhaa ya hatari katika mchezo ambao kocha Slaven Bilic alimtumia kinda wa miaka 16, Reece Oxford akicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England.
Kikosi cha Arsenal; Cech, Debuchy/Sanchez dk67, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin/Walcott dk58, Cazorla, Ramsey, Ozil, Oxlade-Chamberlain na Giroud.
West Ham: Adrian, Tomkins, Reid, Ogbonna, Cresswell, Oxford/Nolan dk79, Noble, Kouyate, .Payet, Zarate/Jarvis dk63, Sakho/Maiga dk89.
Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla akiajribu kuwatoka mabeki wa West Ham Uwanja wa PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment