TIMU ya Arsenal imezinduka na kupata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa mabao 2-1 Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park jioni ya leo.
Mshambuliaji Olivier Giroud alianza kuifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 16, kabla ya beki wa kulia, Joel Ward kuisawazishia Palace dakika ya 28.
Beki Damien Delaney akajifunga dakika ya 55 baada ya kazi nzuri ya Alexis Sanchez kuipatia timu ya Arsene Wenger bao la pili la ushindi linalowapa pointi tatu za kwanza msimu huu.
Kikosi cha Crystal Palace kilikuwa; McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare, Cabaye, McArthur/Bamford dk80, Zaha/Chung-Yong dk76, Puncheon, Bolasie/Mutch dk46 na Wickham.
Arsenal; Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin/Oxlade-Chamberlain dk64, Ramsey, Sanchez/Arteta dk75, Ozil/Gibbs dk83, Cazorla na Giroud.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez akishangilia baada ya jitihada zake kuisaidia timu yake kupata bao la ushindi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment