MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure amerudisha nyumbani kutoka kwenye ziara ya Manchester City nchini Australia baada ya kuumia kichwani kufuatia kugongana na kipa wa Real Madrid, Keylor Navas.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast aligongana vibaya na kipa huyo wa Real aliyeruka kwenye eneo lake kupangua mpira wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo mjini Melbourne jana. Real ilishinda 4-1.
City imeamua kuwarudisha England Toure na kiungo mwenzake, Fabian Delph aliyeumia nyama za paja maana yake wataikosa ziara ya Vietnam.
Yaya Toure amerejeshwa nyumbani kutoka kwenye ziara ya Manchester City baada ya kuumizwa na kipa wa Real Madrid, Keylor Navas jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kuumia kwa wachezaji hao kunaingeza idadi ya majeruhi Man City, baada ya kocha Manuel Pellegrini kusema kwamba mshambuliaji Sergio Aguero na nyota wenzake wa Amerika Kusini wataikosa mechi dhidi ya West Brom Agosti 10 siku kiasi cha wiki moja kabla ya kuvaana na mabingwa, Chelsea.
"Kesho tutajua kutoka kwa daktari, lakini ni vigumu kujua, kwa kuwa daktari anahitaji saa 48," amesema Pellegrini.
Aguero, Pablo Zabaleta, Martin Demichelis na Fernandinho wote wanaweza kukosa mechi za mwanzoni mwa msimu, kwa sababu hawajarejea mazoezini baada ya kumaliza michuano ya Copa America.
0 comments:
Post a Comment