// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
YANGA SC YAWATEMA JAVU, ZAHIR NA KIPA MPYA KIKOSI CHA KAGAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEYANGA SC YAWATEMA JAVU, ZAHIR NA KIPA MPYA KIKOSI CHA KAGAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
YANGA SC YAWATEMA JAVU, ZAHIR NA KIPA MPYA KIKOSI CHA KAGAME
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM YANGA SC haijawajumuisha Mudathir Khamis, Rajab Zahir, Edward Charles na Hussein Javu katika kikosi chake cha wachezaji 20, kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame iliyoanza jana Dar es Salaam. Kipa Mudathir amesajiliwa kutoka KMKM ya Zanzibar, wakati Zahir, Charles na Javu walikuwepo kwenye kikosi cha Yanga SC msimu uliopita. Yanga SC ilianza vibaya kwa kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar e Salaam.
Yanga SC ilianza vibaya kwa kufungwa 2-1 na Gor Mahia jana
Na makocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm na mzalendo Charles Boniface Mkwasa wamewaacha Zahir, Charles na Javu katika kikosi cha Kagame. Majina ambayo Yanga SC imewasilisha Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ajili ya Kagame ya 2015 ni makipa; Ally Mustafa na Deo Munishi ‘Dida’. Mabeki ni Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Kevin Yondani, Joseph Zutah, Oscar Joshua, Mwinyi Haji na Pato Ngonyani. Viungo ni Mbuyu Twite, Simon Msuva, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima, Salum Telela, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuwa, wakati washambuliaji ni Amisi Tambwe, Kpah Sherman, Malimi Busungu na Donald Ngoma. Yanga SC itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na Telecom ya Djibouti Saa 10: 00 jioni mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya Khartoum na KMKM na KCCA na Adama City.
John Bocco (kushoto) akiwania mpira dhidi ya mabeki wa KCCA
Mshambuliaji Mtanzania wa KCCA, Shaaban Kondo (kushoto) akipambana na beki wa Azam FC, Serge Wawa Pascal
Beki wa Azam FC, Erasto Nyoni (kulia) akimtoka beki wa KCCA, Hakim Senkumba
Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy', Hakim Sekumba
Why it's great to see Axel thriving
-
The one-time Reds captain has taken a different path to becoming a
top-flight regular and that's fine, says Sam Carney.
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment