Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imemuuza Mganda Emanuel Okwi kwa Sh. Milioni 250 na ilikuwa mawindoni kuisaka saini ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva- dili ambalo inaonekana sasa ‘limebuma’.
Juzi, Yanga SC imemsainisha Mkataba wa miaka miwili zaidi Msuva- maana yake atakuwa mali ya Jangwani hadi mwaka 2018, kwani Mkataba wake wa sasa unaisha mwakani.
Simba SC inasaka mkali mbadala wa Okwi, baada ya Mganda huyo kusaini Mkataba wa miaka mitano na SonderjyskE FC ya Ligi Kuu ya Denmark mapema wiki hii.
Okwi mwenye umri wa miaka 22, sasa atakuwa analipwa dola za Kimarekani 10,000 kwa mwezi, akipatiwa nyumba, usafiri na huduma nyingine zote muhimu Denmark.
Na Simba SC baada ya kuingiziwa dola za Kimarekani 110,000 inataka kutumia japo robo ya fedha hizo kumpata mchezaji mwingine mkali.
Baada ya Yanga SC kumtia pingu Mchezaji Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, SImba SC watalazimika kuhamishia mawindo yao sehemu nyingine.
Tayari imeelezwa kwamba Simba SC wapo katika mpango wa kusajili mshambuliaji kutoka Brazil, aliyekuwa anacheza Oman.

Simon Msuva (katikati) akisaini Mkataba mpya Yanga SC. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendai, Isaac Chanji na kushoto Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha |
Okwi mwenye umri wa miaka 22, sasa atakuwa analipwa dola za Kimarekani 10,000 kwa mwezi, akipatiwa nyumba, usafiri na huduma nyingine zote muhimu Denmark.
Na Simba SC baada ya kuingiziwa dola za Kimarekani 110,000 inataka kutumia japo robo ya fedha hizo kumpata mchezaji mwingine mkali.
Baada ya Yanga SC kumtia pingu Mchezaji Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, SImba SC watalazimika kuhamishia mawindo yao sehemu nyingine.
Tayari imeelezwa kwamba Simba SC wapo katika mpango wa kusajili mshambuliaji kutoka Brazil, aliyekuwa anacheza Oman.
0 comments:
Post a Comment