Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
MICHUANO ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi wiki hii mjini Dar es Salaam.
Wenyeji, Yanga SC watamenyana na Gor Mahia ya Kenya Saa 10:00 jioni baada ya APR ya Rwanda kupepetana na Al Shandy ya Sudan katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, kuanzia Saa 8:00 mchana.
Mchezo mwingine wa siku hiyo, utafanyika Uwanja wa kumbukumbu ya Karume, Ilala ukizikutanisha KMKM na Telecom ya Djibouyi kuanzia Saa 10:00 jioni.
Waziri wa Miundombinu nchini Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo Julai 18 Uwanja wa Taifa.
Magufuli baada ya kufungua rasmi michuano hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kagame, mechi itakayowakutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya Yanga dhidi ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.
KAGAME 2015 ACHA MOTO UWAKE DAR;
Mchezo wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia unaonekana kuteka hisia za wapenzi wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwani ni takribani miaka 19 timu hizo mbili haziwaji kukutana katika ardhi ya Tanzania.
Mara ya mwisho mwaka 1996 katika michuano ya Cecafa, timu hizo zilikuwa katika kundi moja, katika mchezo wa awali zilitoka sare ya bao 1- 1, wakati zilipokutana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Gor Mahia iliibuka na ushindi wa mabao 4 -0.
Gumzo la wadau wa soka nchini kwa sasa ni kuhusu uwezo wa klabu za Tanzania, Yanga, Azam na KMKM kuweza kuhakikisha kombe la michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki haliondoki kwenye ardhi ya Tanzania.
Lakini zaidi ni kuhusu Yanga SC, iwapo itafanikiwa kutwaa taji hilo mwaka huu, maana yake hiyo itakuwa mara ya sita, hivyo kuwafikia mahasimu wao wa jadi, Simba SC kutwaa mara nyingi Kombe hilo.
Na Yanga wana matumaini ya kulibakiza Kombe kwenye ardhi ya Tanzania kutokana na historia yao nzuri ya miaka ya hivi karibuni pindi Kombe la Kagame linapoandaliwa nchini. Yanga iliibuka kidedea mara mbili mfululizo mwaka 2011 na 2012 mashindano hayo yalipoandaliwa nchini.
Yanga mabingwa mara tano wa michuano hio watakuwa na kazi moja tu ya kujaribu kuifikia rekodi ya Simba, inayoongoza kutwaa Kombe hilo mara nyingi, ikiwa imeweza kufanya hivyo, mara sita.
Yanga iko chini ya mtaalam kutoka Uholanzi, Hans van Pluijm anayesifika kwa kuwa mfuasi asiyetetereka wa soka la kushambulia.
Yanga ina wachezaji kadhaa inaowategemea ili kufanya vizuri. Macho na masikio yataelekezwa kwa Donald Ngoma, mshambuliaji aliyesainiwa kutoka Platinum Fc ya Zimbabwe kuona kama ataendeleza kasi yake ya ufungaji aliyoanza nayo.
Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Nadir Haroub na Amissi Tambwe ni kati ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuendelea kuwa nguzo za Yanga kwenye michuano hii.
Yanga imebahatika kutwaa ubingwa mara tano; (Mwaka 1975, 1993, 1999, 2011, na 2012).
Pia Yanga imemaliza kama washindi wa pili mara mbili, mwaka 1976 ilipofungwa na Gor Mahia 2-1 jijini Kampala na mwaka 1992 ilipolala kwa mikwaju ya penati mbele ya watani wao wa jadi, Simba.
Yanga ilianzishwa mwaka 1935, na kuwa moja ya klabu kongwe kabisa kwenye ukanda huu na bara la Afrika kwa ujumla.
Gor Mahia: Wababe wa Kenya waliojipanga upya kurudisha heshima.
Gor Mahia hawakufanya vizuri katika michuano ya mwaka jana, ila wanatarajiwa kutoa ushindani katika mashindano ya mwaka huu.
Licha ya kupotea kwa muda mrefu kabla ya kuibuka na kushindwa kufurukuta kwenye michauno ya mwaka jana jijini Kigali, Gor Mahia wanajipa moyo Zaidi kutokana na mwenendo wao kwenye Ligi ya Kenya.
Mabingwa hao wa Kenya hawajapoteza mechi msimu huu huku wakionesha dalili za kutangaza ubingwa mapema kabisa.
Kundi lake: Gor Mahia iko kwenye kundi A la michuano ya mwaka huu ikijumuishwa na Yanga, Al Khartoum ya Sudan, KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibout. Ni kundi ambalo ni gumzo kuu likdaiwa kuwa na mechi zenye msisimko Zaidi na ushindani mkubwa.
Kwa wafuatiliaji wa soka nchini Kenya, hakuna anayepinga kuwa kwa sasa timu yenye wachezaji bora zaidi ni Gor Mahia.
Wachezaji kama Khalid Aucho, chipukizi Micheal Olunga anayetajwa kuwa mrithi wa mshambuliaji bora kuwahi kutokea nchini Kenya, Dennis Oliech, na Meddie Kagere wamekuwa ni kiungo muhimu kwenye timu hii.
Wachezaji wengine ni pamoja na mlinda mlango Boniface Oluoch zake kutikiswa kwenye ligi ya Kenya inayoendelea kwa sasa.
Mlinzi wa Uganda Cranes, Godfrey Walusimbi na George Odhiambo wakiongeza chachu kwenye timu hiyo.
Gor Mahia inaongozwa na kocha Frank Nuttal, raia wa Uskochi. Benchi lao la ufundi linajumuisha pia mlinda mlango wa zamani wa kimataifa wa Harambe Stars, Mathew Ottamax ambaye ana jukumu la kuwanoa walinda mlango, Boniface Oluoch na Jerim Onyango.
Mara ya mwisho Gor Mahia ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1985, lakini imetwaa ubingwa huo mara 5 (1976, 1977, 1980, 1981, 1985).
Mwandishi wa makala haya ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambaye anapatikana kwa namba +255 713 455970 au barua pepe b.kizuguto@tff.or.tz)

Kikosi cha Yanga SC kilichotwaa Kombe la Kagame mwaka 1993 mjini Kampala, Uganda |

0 comments:
Post a Comment