Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC leo asubuhi wanaingia kambini katika hosteli za Chuo Cha Maaskofu, Kurasini mjini Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Wachezaji wa Yanga SC jana walilala katika hoteli ya valley View, Mtaa wa Kongo, Kariakoo, Dar es Salaam na leo asubuhi wanaingia kambi hiyo ya Chuo cha Maaskofu.
Yanga SC ambayo imepangwa Kundi A pamoja na Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibouti, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan, itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini.
Na uongozi umesema katika mazoezi hayo hataruhusiwa shabiki wala Mwandishi wa Habari kuingia kwa sababu hilo ndilo sharti walilopewa na uongozi wa chuo hicho.
Mabingwa mara tano wa michuano hiyo, 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012, watafungua dimba na Gor Mahia Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo itatanguliwa na mchezo kati ya APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan Saa 8:00 mchana.
Mchezo mwingine utafanyika Uwanja wa Karume Jumamosi baina ya KMKM na Telecom Saa 10:00 jioni, muda ambao pia Yanga watakuwa wanapepetana na Gor Mahia.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia na Kundi C kuna Azam FC wa Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.

Makocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm (kushoto) na Charles Boniface Mkwasa (kulia) |
Na uongozi umesema katika mazoezi hayo hataruhusiwa shabiki wala Mwandishi wa Habari kuingia kwa sababu hilo ndilo sharti walilopewa na uongozi wa chuo hicho.
Mabingwa mara tano wa michuano hiyo, 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012, watafungua dimba na Gor Mahia Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo itatanguliwa na mchezo kati ya APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan Saa 8:00 mchana.
Mchezo mwingine utafanyika Uwanja wa Karume Jumamosi baina ya KMKM na Telecom Saa 10:00 jioni, muda ambao pia Yanga watakuwa wanapepetana na Gor Mahia.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia na Kundi C kuna Azam FC wa Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.
0 comments:
Post a Comment