Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KMKM ya Zanzibar na Yanga SC hatimaye zimefikia makubalino juu ya mlinda mlango Mudathir Khamis.
Kipa huyo namba Zanzibar alimalizana na Yanga SC mwezi uliopita, lakini klabu yake, KMKM ikaweka ngumu hivyo akashindwa kujiunga na timu yake mpya.
Lakini leo, Katibu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwamba suala hilo limemalizwa.
“Sisi na KMKM tumemalizana kiungwana juu ya kipa huyu (Mudathir). Sasa naweza kusema Mudathir yuko huru kujiunga na Yanga SC kwa Mkataba wa miaka miwili,”amesema Dk. Tiboroha, ambaye utendaji wake unawafurahisha wana Yanga wengi.
Mudathir sasa atajiunga na kambi ya Yanga SC inayojiandaa na michauno ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, inayotarajiwa kuanza Jumamosi, Dar es Salaam.
Yanga SC leo asubuhi wanaingia kambini katika hosteli za Chuo Cha Maaskofu, Kurasini mjini Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Yanga SC ambayo imepangwa Kundi A pamoja na Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan, itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini.
Mabingwa mara tano wa michuano hiyo, 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012, watafungua dimba na Gor Mahia Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo itatanguliwa na mchezo kati ya APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan Saa 8:00 mchana.
Mchezo mwingine utafanyika Uwanja wa Karume Jumamosi baina ya KMKM na Telecom Saa 10:00 jioni, muda ambao pia Yanga watakuwa wanapepetana na Gor Mahia.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia na Kundi C kuna Azam FC wa Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.

Mudathir Khamis sasa ni mali ya Jangwani, baada ya Yanga SC kumalizana na KMKM |

0 comments:
Post a Comment