// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC, GOR MAHIA HAWATISHI- BUSHIRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC, GOR MAHIA HAWATISHI- BUSHIRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 17, 2015

    YANGA SC, GOR MAHIA HAWATISHI- BUSHIRI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa KMKM ya Zanzibar, Ally Bushiri (pichani) amesema kwamba hakuna timu inayomuumiza kichwa katika Kundi A michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
    Bushiri maarufu kama Bush, amesema kwamba anazifahamu vyema timu zote katika kundi lao na haoni hata moja ya kumsumbua.
    KMKM imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji Yanga SC, Telecon ya Djibouti na Gor Mahia ya Kenya. 
    KMKM itafungua dimba na Telecom Saa 8:00 mchana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Saa 10: 00 jioni Yanga watapepetana na Gor Mahia na Uwanja wa Karume APR ya Rwanda itamenyana na Al Shandy ya Sudan, mchezo wa Kundi B.  
    Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye hivi karibuni ameteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Oktoba mwaka huu atakuwa mgeni rasmi katika mechi za ufunguzi Uwanja wa Taifa.
    Na kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Bushiri amesema kwamba hakuna timu ya kuogopa wala kudharau kwa sababu kiwango cha soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati hakitofautiani sana.
    “Kwa mitazamo ya haraka haraka, watu wanaweza wakasema Yanga na Gor Mahia wanatisha na wakatuona kama sisi (KMKM) na wale wa Djibouti kama wasindikizaji, kumbe sivyo. Mpira hauko hivyo,”amesema Bushiri na kuongeza.
    “Mimi nina uzoefu na soka yetu kuanzia kwenye kucheza hadi kufundisha kwa ngazi ya klabu na hata timu za taifa. Ninazijua vizuri timu karibu zote katika mashindano haya, niseme tu tumekuja Dar es Salaam kuwania Kombe la Kagame mwaka 2015,”.
    Bushiri amesema vijana wake wako vizuri kabisa kuelekea michuano hiyo na amewataka wapenzi wa soka Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kesho kushuhudia burudani nzuri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC, GOR MAHIA HAWATISHI- BUSHIRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top