Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa ufungzuzi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe Kagame kati ya Yanga SC na Gor Mahia ya Kenya Jumamosi kitakuwa Sh. 5,000 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waandaji wa michuano hiyo, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wametaja viingilio vya hatua ya makundi.
Michezo ya Uwanja wa Karume kiingilio kitakua Sh. 2,000 na Uwanja wa Taifa Sh. 5,000 na majukwaa ya VIP ni Sh 20,000.
Kombe la Kagame Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka 1967 kwa kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu ni mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo
Klabu ya Simba ndio timu inayoongzoa kwa kutwaa ubingwa huo mara sita (6) ikifuatiwa na Yanga, Gor Mahia zilizotwa mara (5), APR ya Rwanda ikiwa imetwaa ubingwa huo mara tatu (3). Yanga na Gor Mahia zina nafasi ya kufikia Simba SC endapo zitafanikiwa kutwaa Ubingwa msimu huu.
Mechi ya ufunguzi ufunguzi siku ya jumamosi uwanja wa Taifa itawakutanisha APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan saa 8 kamili mchana, KMKM kutoka Visiwani Zanzibar watacheza dhidi ya Telecom ya Djibout Uwanja wa Karume saa 10 jioni, huku wenyeji timu ya Yanga wakiwakaribisha Gor Mahia kutoka Kenya saa 10 jioni.
Timu zinazoshiriki michuano hiyo, Kundi A; Yanga (Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Kundi B: APR (Rwanda), Al-Shandy (Sudan),LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia) na Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda).
Michuano hiyo ya CECAFA Kagame Cup itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha Supersport.

0 comments:
Post a Comment