// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WANGA AANZA MAZOEZI AZAM FC, ‘MIDO’ WA ENGLAND SASA HATARINI KUTEMWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WANGA AANZA MAZOEZI AZAM FC, ‘MIDO’ WA ENGLAND SASA HATARINI KUTEMWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 17, 2015

    WANGA AANZA MAZOEZI AZAM FC, ‘MIDO’ WA ENGLAND SASA HATARINI KUTEMWA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Kenya, Alan Watende Wanga leo amefanya mazoezi na Azam FC kwa mara ya kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam- maana yake ameitikia wito wa kocha Muingereza, Stewart Hall.
    Hall alisema hawezi kusajili mchezaji bila kumuona mazoezini na suala la Wanga lilikuwa kwenye utata- hatimaye amelazimika kufuata masharti ya Muingereza huyo.
    Na Hall alikuwa ana sababu za msingi juu ya uamuzi wake huo; “Nahitaji kumuona mchezaji kwa sababu nyingi, nione uwezo wake kwa wakati huu, nijue kama yuko fiti, nione namna ambavyo anashirikiana na wenzake. Sitaki kukaribisha matatizo katika chumba cha kubadilishia nguo,”alisema Hall akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE wiki hii.
    Alan Wanga (katikati) akifanya mazoezi na Azam FC leo Chamazi

    Sasa Wanga aliyemaliza Mkataba wake El Marreikh ya Sudan Juni mwaka huu, anaweza kukamilisha idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye kikosi cha Azam FC, kabla ya kuanza kwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kesho.
    Atakuwa mchezaji wa pili mpya wa kigeni kusajiliwa katika dirisha hili, baada ya kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ kutoka APR ya kwao, ambao kwa pamoja wanaungana na beki Serge Wawa Pascal, kiungo Kipre Michael Balou, mshambuliaji Kipre Tchetche wote kutoka Ivory Coast, winga Brian Majwega kutoka Uganda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi ambao wote walikuwepo msimu uliopita.
    Wachezaji wengine wa kigeni wanaowania kusajiliwa Azam FC katika nafasi moja iliyobaki ni kipa Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast na kiungo Ryan Burge kutoka England.
    Awali, Azam FC ilisajili wazalendo tu wawili ambao ni kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Simba SC na Ame Ali ‘Zungu’ kutoka Mtibwa Sugar.
    Azam FC iliyoingia kambini leo katika hosteli zao za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam imepangwa Kundi C pamoja na Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.
    Itafungua dimba na KCCA Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Saa 10: 00 jioni mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Adama City na Malakia utakaonza Saa 8:00 mchana, wakati jioni Saa 10:00 Uwanja wa Karume, LLB AFC itamenyana na Hegaan FC.
    Mechi za utangulizi Jumamosi zitakuwa kati ya 
    KMKM na Telecom, APR  na Shandy na Yanga na Gor Mahia. 
    APR ipo Kundi B pamoja na Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia na Kundi A kuna wenyeji, Yanga SC, Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan, 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WANGA AANZA MAZOEZI AZAM FC, ‘MIDO’ WA ENGLAND SASA HATARINI KUTEMWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top