MSHAMBULIAJI Robin van Persie ametambulishwa katika klabu yake mpya, Fenerbahce leo jioni katika sherehe za kusaini kwake kutoka Manchester United.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 31 aliwasili mjini Istanbul mwishoni mwa wiki kukamilisha uhamisho wake na leo ametambulishwa Uwanja wa Sukru Saracoglu ambako alisaini fomu za mshahara wa Pauni 240,000 kwa wiki mbele ya maelfu ya mashabiki.
"Ninafurahi kuona mashabiki wengi babu kubwa namna hii wamekuja leo kunisalimia na kunikaribisha katika familia yao,"amesema Mholanzi huyo mbele ya umari.
Robin van Persie akiusalimia umati wa mashabiki wa Fenerbahce baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment