Na Mwandishi Wetu, Morogoro
CHAMA cha Soka Morogoro (MRFA) kimeanza kutoa fomu za kugombea nafasi mbalimbali,ambapo aliyewahi kuwa katibu wake ,Aristo Nikitas amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ukatibu kwa mara nyngine tena,huku nmwandishi wa habari wa wa gazeti la Nipashe mkaoni hapa Ashton Balaigwa akitangaza kuwania nafasi ya Uenyekiti.
Uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu,Morogoro,MRFA unatarajiwa kutafanyika Agosti 9 mwaka huu,utaratibu wa kutoa fomu umeanza kutolewa ofisi za MRFA zilizopo uwanja wa Jamhuri mjini hapa na siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo kwa wagombea ni julai 07 mwaka huu.
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu (MRFA), Aristo Nikitas akitoka katika ofisi za chama hicho kuchukua fomu kwajili ya kuwania tena nafasi hiyo katika uchaguzi unaotalajia kufanyika Agosti 9 mwaka huu
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Aristo Nikitas alisema kilichomrudisha kugombea nafasi hiyo ni baada ya kuona soka la mkoa linashuka kila siku na anaamini kuwa kama atarudi tena madarakani atashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha soka linarudi.
Nikitas alisema atashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha vyama vya wilaya vinasimama na kuweza kuendesha soka,pamoja na kuweza kunyanyua vipaji vingi vya soka ambavyo vipo lakini hakuna anayejali vijana hao.
Kwa upande wake Balaigwa alisema ameahamua kujitokea kuwania nafasi hiyo ili kulerta chache ya maerndelero na kurudisha adhai ya soka kimkoa kwani kwa sasa imelala.
Balaigwa alisema kuwa kwa kutumia tasnia ya habari kwa kushirikiana na viongozi wataokachaguliwa ataleta mabadiliko makubwa katika soka la mkoa,akiamini kuwa wanahabari wote watakuwa mstari wa mbele kutetea soka la mkoa wa morogoro.
Mgombea wa kwanza aliyeanza kuchukua fomu ni Katibu Msaidizi wa MRFA kwa sasa,Emanuel Kimbawala ambaye nae anawania nafasi ya Katibu,Ramadhani Wagala anagombea nafasi ya mjumbe wa uwakilishi wa vilabu TFF,huku waliotangaza nia ya kupata uongozi katika chama hicho ni pamoja na Nickson Mkilanya nafasi ya uwakilishi wa vilabu vya soka kwenye mkutano mkuu wa TFF.
Katika uchaguzi huo jumla ya nafasi nane za uongozi zitagombewa,ambazo ni Mwenyekiti ,Makamu Mwenyekiti,Katibu,Katibu Msaidizi,Mweka Hazina,Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF,Mjumbe Mwakilishi wa Vilabu TFF na Wajumbe watatu wa kamati ya Utendaji.
Tayari wachambuzi wa mchezo wa soka mkoani hapa,wanasema uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na ushindani mkubwa, kutokana na sifa zilizowekwa, sambamba na wagombea wanaojitokeza kuonekana kuwa na uwezo mkubwa katika soka.
Mwisho.

0 comments:
Post a Comment