TANZANIA imeporomoka kwa nafasi 12 hadi ya 139 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hiyo inafuatia matokeo mabaya mfululizo mwezi uliopita kuanzia kwenye Kombe la COSAFA ambako ilifungwa mechi zote tatu za Kundi B, mechi ya kwanza kufuzu AFCON ilipochapwa 3-0 na Misri kabla ya kutolewa kwa mabao 4-1 na Uganda kufuzu CHAN 2016.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimfukuza kocha Mholanzi, Mart Nooij baada ya matokeo hayo na nafasi yake sasa anakaimu, Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ambaye amepewa miezi mitatu ya majaribio.
Mkwasa ameanza vizuri baada ya kupata sare ya ugenini ya 1-1 na Uganda katika mchezo wa marudiano kufuzu CHAN, kufuatia kipigo cha 3-0 Zanzibar chini ya Nooij.
Katika orodha iliyotolewa leo na FIFA mjini Zurich, Uswisi, ‘Wababe wetu’, Uganda nao wameporomoka kwa nafasi mbili hadi ya 73, ingawa wanaongoza kwa ubora kwa nchi wanachama wa CECAFA.
Rwanda imeporomoka kwa nafasi 16 hadi ya 78, Sudan imeporomoka kwa nafasi 18 hadi ya 90, wakati Algeria bado inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa nafasi ya 19.
Argentina pamoja na kufungwa kwenye fainali ya Copa America bado inaongoza ikifuatiwa na mabingwa wa dunia, Ujerumani, Ubelgiji, Colombia na Uholanzi.

Kocha Mart Nooij akisindikizwa na Polisi kutoka Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya Taifa Stars kufungwa 3-0 na Uganda |
Mkwasa ameanza vizuri baada ya kupata sare ya ugenini ya 1-1 na Uganda katika mchezo wa marudiano kufuzu CHAN, kufuatia kipigo cha 3-0 Zanzibar chini ya Nooij.
Katika orodha iliyotolewa leo na FIFA mjini Zurich, Uswisi, ‘Wababe wetu’, Uganda nao wameporomoka kwa nafasi mbili hadi ya 73, ingawa wanaongoza kwa ubora kwa nchi wanachama wa CECAFA.
Rwanda imeporomoka kwa nafasi 16 hadi ya 78, Sudan imeporomoka kwa nafasi 18 hadi ya 90, wakati Algeria bado inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa nafasi ya 19.
Argentina pamoja na kufungwa kwenye fainali ya Copa America bado inaongoza ikifuatiwa na mabingwa wa dunia, Ujerumani, Ubelgiji, Colombia na Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment