// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TANZANIA NA ZAMBIA KIINGILIO KARIBU NA BURE KESHO CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TANZANIA NA ZAMBIA KIINGILIO KARIBU NA BURE KESHO CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 10, 2015

    TANZANIA NA ZAMBIA KIINGILIO KARIBU NA BURE KESHO CHAMAZI

    TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 (Tanzanite) kesho siku ya jumamosi itashuka dimbani uwanja wa Azam Complex kucheza na timu ya Taifa ya Zambia chini ya miaka 20 (Young She-Polopolo).
    Viingilio vya mchezo wa kesho kati ya Tanzanite dhidi ya Young She-Polopolo ni shilingi elfu mbili (2,000/=) kwa jukwaa la mzunguko, na shilingi  elfu tatu (3,000/=) kwa Jukwaa Kuu.
    Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Papua New Guinea, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Sudan,unatarajiwa kuanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kati.
    Timu ya Young She-Polopolo tayari imeshwasili nchini jana jioni, na leo wakitarajiwa kufanya mazoezi mepesi leo jioni katika uwanja wa Azam Complex kw ajaili ya mchezo huo. Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Sudan tayari wameshawasili.
    Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetoa usafiri wa mabus mawili kwa ajili ya kikundi cha ushangiliaji cha timu za Taifa (Taifa Supporters) kitachokwenda kesho Chamazi kuipa sapoti timu ya Tanzanite.
    Mabasi hayo mawili yataondoka ofisi za TFF zilizopo Karume saa 6 kamili mchana kuelekea Chamazi kwa ajili ya kuishangilia timu ya Taifa ya wanawake  chini ya miaka 20 (Tanzanite).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA NA ZAMBIA KIINGILIO KARIBU NA BURE KESHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top