// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STEWART ASEMA MESSI, BALOU, TCHETCHE, AME, WAWA WOTE ‘WAPO UNGA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STEWART ASEMA MESSI, BALOU, TCHETCHE, AME, WAWA WOTE ‘WAPO UNGA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, July 15, 2015

    STEWART ASEMA MESSI, BALOU, TCHETCHE, AME, WAWA WOTE ‘WAPO UNGA’

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    NYOTA wa Azam FC, Serge Wawa Pascal Kipre, Miachel Balou, Kipre Herman Tchetche wote raia wa Ivory Coast pamoja wazalendo Ramadhani Singano ‘Messi’ na Ame Ali ‘Zungu’ wote hawako fiti.
    Hayo yamesemwa na kocha Mkuu wa timu hiyo Muingereza, Stewart John Hall katika mahojiano na BIN ZUNBEIRY SPORTS- ONLINE jana jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Pamoja na hao, Stewart amesema wachezaji wawili pia waliokuja majaribio kipa Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast na kiungo Ryan Burge kutoka England, pia hawako fiti.
    Na wakati michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inaanza Jumamosi Dar es Salaam, Stewart amesema kwamba wachezaji wake kadhaa tegemeo hawako tayari. 
    Hawako fiti; Kipre Tchetche (kulia) na Ramadhani Singano 'Messi' kushoto wakifanya mazoezi maalum baada ya kumaliza programu ya timu jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

    Stewart amevutiwa na Burge na amempa programu maalum ya kumuweka fiti pamoja na Wawa, Balou, Tchetche, Messi na Ame ambao wote wamekuwa wakifanya mazoezi ya ziada kabla na bada ya mazoezi ya timu kwa ujumla.
    “Siku chache zimebaki kabla ya Kagame, lakini wachezaji wengi tegemeo katika kikosi cha kwanza hawako fiti. Messi, Kipre Tchetche, Balou, Ame, Serge Wawa na Ryan wote hawako fiti kwa sababu walichelewa kujiunga na wenzao kwa maandalizi ya mwanzo wa msimu,”amesema.
    Hata hivyo, mtaalamu huyo amesema atafanya jitihada zinazowezekana kuhakikisha kwa siku chache zilizobaki wachezaji hao wanakuwa fiti angalau kwa asilimia 50.
    Stewart Hall (katikati) akijadiliana na Meneja wa Azam FC, Luckson Kakolaki na kipa wa timu ya vijana, Metacha Boniphace
    Kipre Michael Balou hayuko fiti
    Serge Wawa Pascal pia hayuko fiti

    “Napambana kupata angalau asilimia 50, kama wakizidi hapo itakuwa vizuri. Lakini lengo ni kufanya vizuri katika haya mashindano, ikibidi kuchukua Kombe,”amesema. 
    Aidha, Stewart amepongeza usajili wa kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ kutoka APR ya kwao, akisema ni mchezaji mzuri kwa ujumla.
    Migi anakuwa mchezaji wa sita wa kigeni wa Azam kati ya saba wanaotakiwa- na wa kwanza kabisa mpya kusajiliwa msimu huu. Wachezaji wa kigeni waliopo Azam FC ni beki Serge Wawa Pascal, kiungo Kipre Michael Balou, mshambuliaji Kipre Tchetche wote kutoka Ivory Coast, winga Brian Majwega kutoka Uganda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi ambao wote walikuwepo msimu uliopita.
    Jean Baptiste Mugiraneza amefikisha idadi ya wachezaji sita wa kigeni waliosajiliwa Azam FC

    Lakini pia, kuna wachezaji wengine wanne wa kigeni wanawania kusajiliwa Azam FC katika nafasi moja iliyobaki, ambao ni makipa Nelson Lukong kutoka Cameroon, Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast, kiungo Ryan Burge kutoka England na mshambuliaji Allan Wetende Wanga kutoka Kenya.
    Lukong na Wanga wamegoma kufanya majaribio na kocha Muingereza Stewart Hall amesema hatasajili mchezaji ambaye hajamuona mazoezini- hivyo nafasi hiyo inaweza kuchukuliwa na Burge anayaendelea na majaribio, kwani hata kipe mwingine Angban anaonekana wa kawaida.
    Awali, Azam FC ilisajili wazalendo tu wawili ambao ni kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Simba SC na Ame Ali ‘Zungu’ kutoka Mtibwa Sugar.
    Azam imepangwa Kundi C pamoja na Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda, wakati Kundi A kuna wenyeji wengine, Yanga SC, Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan na Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STEWART ASEMA MESSI, BALOU, TCHETCHE, AME, WAWA WOTE ‘WAPO UNGA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top