Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaweza kwenda kuweka kambi Uturuki mwezi ujao kujiandaa na mchezo wa pili wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon dhidi ya Nigeria.
BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE inafahamu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi anahaha kuhakikisha zinapatikana fedha za kuipeleka timu Uturuki kwa kambi japo ya wiki mbili.
Na Stars inatarajiwa kwenda Uturuki baada ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza wiki ijayo Dar es Salaam.
Taifa Stars ilianza vibaya kampeni za Gabon 2017, baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Misri mjini Alexandria katikati ya mwezi uliopita na sasa inaelekeza nguvu zake kusaka pointi tatu za kwanza katika mchezo wa kwanza Septemba.
Aliyekuwa kocha wa Taifa Stars tangu Aprili mwaka jana, Mholanzi Mart Nooij alifukuzwa kazi mwishoni mwa mwezi uliopita kutokana na matokeo mabaya, ikiwemo kufungwa mechi tano mfululizo na nafasi yake sasa anakaimu kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa.
Stars ambayo iliweka kambi ya wiki moja Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kucheza na Misri Juni 14, itashuka dimbani tena Jumamosi ya Septemba 5, kumenyana na Nigeria mjini Dar es Salaam kabla ya kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza za Kundi G kwa kumenyana na Chad Machi 25 mwakani.
Malinzi ana kiu kubwa ya kuirejesha Tanzania kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika, ambazo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza mwaka 1980- na ndiyo maana amekuwa akihakikisha maandalizi yanakuwa mazuri.

0 comments:
Post a Comment