Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
MWANDISHI wa habari mwandamizi wa michezo Tanzania, Somoe Ng’itu amepita katika mchujo wa awali kuelekea Uchaguzi wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (TWFA).
Kamati ya Uchaguzi ya TWFA imemtaja Somoe anayeandikia gazeti la Nipashe kwamba amepita katika nafasi ya Katibu Msaidizi, akichuana na Cecilia Makafu.
Waliopita nafasi ya Mwenyekiti ni Amina Ali Karuma na Devotha John Marwa, wakati Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Debora Ernest Mkemwa, Mwanaheri Kalolo na Theresia Reginald.
TWFA imemtaka mtu yeyote mwenye pingamizi kwa mgombea yeyote kuliwasilisha katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam kuanzia kuanzia Julai 15 hadi Julai 20 siku ya usajili wa wagombea.

Somoe kulia akiwa wifi yake, Dina katika moja ya hafla kubwa nchini |
TWFA imemtaka mtu yeyote mwenye pingamizi kwa mgombea yeyote kuliwasilisha katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam kuanzia kuanzia Julai 15 hadi Julai 20 siku ya usajili wa wagombea.
0 comments:
Post a Comment