// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC WAHAMISHIA KAMBI YAO ZENJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC WAHAMISHIA KAMBI YAO ZENJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, July 19, 2015

    SIMBA SC WAHAMISHIA KAMBI YAO ZENJI

    Na Princess Aasia, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa zamani wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati, Simba SC kesho wanatarajiwa kuhamishia kambi yao Zanzibar.
    Simba SC wamerejea leo Dar es Salaam kutoka Lushoto, Tanga walipokuwa wameweka kambi kwa wiki mbili zilizopita na moja kwa moja kwenda Zanzibar kuendelea na maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayoanza Septemba. 
    Washindi hao wa pili wa Kombe la CAF (sasa Shirikisho) mwaka 1993, wanatarajiwa kurejea tena Dar es Salaam mwezi ujao kwa ajili ya mchezo wa kirafiki katika tamasha la Simba Day dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

    Kikosi cha Kocha Muingereza, Dylan Kerr kikaendelea kilichokwenda Zanzibar ni makipa; Peter Manyika, David Robert Kisu, Denis Deonis Richard na Ivo Mapunda, mabeki, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Samih Hajji Nuhu, Hassan Isihaka, Murushid Juuko na Mohamed Fakih Khatib.
    Viungo ni Jonas Mkude, Said Ndemla, 
    Abdi Banda, Awadh Juma, Simon Sserenkuma, Peter Mwalyanzi na washambuliaji Mussa Hassan Mgosi, Ibrahim Hajib, Hamisi Kiiza, Elias Maguli, Issa Abdallah Ngoa, Emmanuel Alex Massawe, Michael Mgimwa, Mbaruku Yusuph na Saidi Issa.
    Benchi la ufundi limeongozwa na kocha Mkuu, Dylan Kerr, Kocha Msaidizi, Suleiman Matola, Kocha wa makipa Iddi Salim Abdul, Kocha wa viungo, Dusan Momcilovic na Daktari Yassin Gembe.
    Wachezaji wa Simba SC walikuwepo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo wakati mechi za ufunguzi Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wakiwashudhia wapinzani wao, Yanga SC wakifungwa 2-1 na Gor Mahia ya Kenya.
    Kufanya vibaya kwa Simba SC kwa miaka mitatu iliyopita katika Ligi Kuu, kumewafanya siyo tu wakose nafasi ya kucheza Kombe la Kagame, bali hata michano ya Afrika, yaani Kombe la Washindi na Ligi ya Mabingwa. 
    Lakini msimu huu, chini ya Rais wake, Evans Elieza Aveva- Simba SC imepania kurejesha heshima.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAHAMISHIA KAMBI YAO ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top