MSHAMBULIAJI Raheem Sterling amesaini Mkataba wa miaka mitano Manchester City.
Kinda huyo amekamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 49 kutoka Liverpool kwenda Manchester City baada ya kufaulu vipimo vya afya leo na kocha Manuel Pellegrini amesema kumsajili Sterling maana yake amepata moja ya wachezaji wazuri wa ushambuliaji katika dunia ya soka.
Kinda huyo amekamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 49 kutoka Liverpool kwenda Manchester City baada ya kufaulu vipimo vya afya leo na kocha Manuel Pellegrini amesema kumsajili Sterling maana yake amepata moja ya wachezaji wazuri wa ushambuliaji katika dunia ya soka.
"Raheem Sterling ni mmoja wa wachezaji wazuri wa ushambuliaji katika dunia ya soka, na ninataka sana ajiunge na kikosi katika ziara ya Australia baadaye wiki hii,"amesema Pellegrini.
Mwanasoka huyo wa kimaataifa wa England akiwa na nyota wa kike wa City, Krystle Johnston (kushoto) na Toni Duggan (kulia) PICHA ZAIDI GONGA HAPA
City iligonga mwamba katika ofa zake mbili za awali juu ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amepigwa picha akitoka kwenye hospitali ya Manchester kabla ya kufikia makubaliano mwishoni mwa wiki.
WACHEZAJI GHALI ZAIDI LIGI KUU ENGLAND
1. Angel di Maria (Man United) Pauni Milioni 60
2. Fernando Torres (Chelsea) Pauni Milioni 50
3. RAHEEM STERLING (Man City) Pauni Milioni 49
4. Mesut Ozil (Arsenal) Pauni Milioni 42.5
5. Sergio Aguero (Man City) Pauni Milioni 38
6. Juan Mata (Man United) Pauni Milioni 37
7. Andy Carroll (Liverpool) Pauni Milioni 35
8. Alexis Sanchez (Arsenal) Pauni Milioni 35
9. Fernandino (Man City) Pauni Milioni 34
10. Robinho (Man City) Pauni Milioni 32.5
HAWA NDIO WACHEZAJI GHALI ZAIDI DUNIANI
1. Gareth Bale (Real Madrid) Pauni Milioni 85.3
2. Cristiano Ronaldo (Real Madrid) Pauni Milioni 80
3. Luis Suarez (Barcelona) Pauni Milioni 75
4. Neymar (Barcelona) Pauni Milioni 75
5. James Rodriguez (Real Madrid) Pauni Milioni 63
6. Angel di Maria (Man United) Pauni Milioni 59.7
7. Zlatan Ibrahimovic (Barcelona) Pauni Milioni 59
8. Kaka (Real Madrid) Pauni Milioni 56
9. Edinson Cavani (PSG) Pauni Milioni 55
10. Radamel Falcao (Monaco) Pauni Milioni 51
City wamewalipa wapinzano wao hao katika Ligi Kuu ya England Pauni Milioni 49, wakati Sterling atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 180,000 kwa wiki, huo uhamisho wa saba wa bei kubwa kuhusisha klabu za Uingereza.
Sterling, ambaye Mkataba wake Liverpool ulikuwa unamalizika mwaka 2017, atakuwa mchezaji ghali zaidi wa England kihistoria.
Tathmini za karibuni zilimuweka mchezaji huyo katika thamani ya mchezaji ghali zaidi mdogo katika soka ya Ulaya, akifuatiwa na beki wa Paris Saint-Germain, Marquinhos na mchezaji mpya wa Manchester United, winga Memphis Depay.
0 comments:
Post a Comment