Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefunga mabao mawili moja kwa kazi nzuri ya ‘nduguye’ Thomas Emmanuel Ulimwengu jana TP Mazembe ikiichapa 8-1 Raja Tangier ya Daraja la Tatu Morocco katika mchezo wa kirafiki mjini Tangier.
Katika mchezo huo uliofuatia sare ya 0-0 dhidi ya wenyeji Moghreb Tetouan mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Raja walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita.
Makosa ya Nahodha Kimwaki ndiyo yaliwagharimu Mazembe kufungwa mapema, baada ya pasi yake kunaswa na Azam Anware aliyemtungua kipa Robert Muteba Kidiaba.
Lakini ‘The Ravens’ wakafanikiwa kusawazisha dakika ya 12 kupitia kwa Samatta aliyeweka mpira kifuani kabla ya kufumua shuti, kufuatia krosi ya Mtanzania mwenzake, Thomas Ulimwengu.
Sama Goal tena akawafungia Mazembe bao la pili dakika ya 25 akimalizia kazi nzuri ya Rainford Kalaba.
Kipindi cha kwanza, Mazembe walitoka wanaongoza 2-1 na kipindi cha pili ndipo walipotengeneza ushindi mtamu wa 8-1.
Ousmane Cisse alifunga la tatu dakika ya 56 akimalizia pasi ya Gladson Awako, Ali Sadiki akafunga la nne akimalizia pasi ya Yaw Frimpong dakika ya 68, Given Singuluma akafunga la tano akimalizia kazi nzuri ya Ali Sadiki dakika ya 75. Mabao mengine yalifungwa na Jonathan Bolingi dakika za 70 na 79 kwa pasi za Gladson Awako na Yannick Tusilu na Cheibane Traore kwa penalti baada ya Ali Sadiki kuchezewa rafu dakika ya 77.
Mazembe wataendelea kubaki mjini Tangier hadi katikati ya wiki ijayo watakaposafiri hadi Alexandria, Misri ambako watamenyana na wenyeji Smouha SC Ijumaa ya Julai 24 katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A mzunguko wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika Saa 1:00 usiku.
Mazembe imetoa sare ya bila mabao katika mechi zake zote mbili za awali, kwanza nyumbani la El Hilal ya Sudan na baadaye Morocco dhidi ya Moghreb Tetouan.
Al Hilal ya Sudan ndiyo inaongoza Kundi A kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Smouha pointi tatu, wakati Mazembe ina pointi mbili na Moghreb Tetouan ya Morocco yenye pointi moja inashika mkia.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefunga mabao mawili moja kwa kazi nzuri ya ‘nduguye’ Thomas Emmanuel Ulimwengu jana TP Mazembe ikiichapa 8-1 Raja Tangier ya Daraja la Tatu Morocco katika mchezo wa kirafiki mjini Tangier.
Katika mchezo huo uliofuatia sare ya 0-0 dhidi ya wenyeji Moghreb Tetouan mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Raja walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita.
Makosa ya Nahodha Kimwaki ndiyo yaliwagharimu Mazembe kufungwa mapema, baada ya pasi yake kunaswa na Azam Anware aliyemtungua kipa Robert Muteba Kidiaba.
Lakini ‘The Ravens’ wakafanikiwa kusawazisha dakika ya 12 kupitia kwa Samatta aliyeweka mpira kifuani kabla ya kufumua shuti, kufuatia krosi ya Mtanzania mwenzake, Thomas Ulimwengu.
Mbwana Samatta (kushoto) jana mjini Tangier ambako alifunga mabao mawili |
Sama Goal tena akawafungia Mazembe bao la pili dakika ya 25 akimalizia kazi nzuri ya Rainford Kalaba.
Kipindi cha kwanza, Mazembe walitoka wanaongoza 2-1 na kipindi cha pili ndipo walipotengeneza ushindi mtamu wa 8-1.
Ousmane Cisse alifunga la tatu dakika ya 56 akimalizia pasi ya Gladson Awako, Ali Sadiki akafunga la nne akimalizia pasi ya Yaw Frimpong dakika ya 68, Given Singuluma akafunga la tano akimalizia kazi nzuri ya Ali Sadiki dakika ya 75. Mabao mengine yalifungwa na Jonathan Bolingi dakika za 70 na 79 kwa pasi za Gladson Awako na Yannick Tusilu na Cheibane Traore kwa penalti baada ya Ali Sadiki kuchezewa rafu dakika ya 77.
Mazembe wataendelea kubaki mjini Tangier hadi katikati ya wiki ijayo watakaposafiri hadi Alexandria, Misri ambako watamenyana na wenyeji Smouha SC Ijumaa ya Julai 24 katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A mzunguko wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika Saa 1:00 usiku.
Mazembe imetoa sare ya bila mabao katika mechi zake zote mbili za awali, kwanza nyumbani la El Hilal ya Sudan na baadaye Morocco dhidi ya Moghreb Tetouan.
0 comments:
Post a Comment