MAMIA ya mashabiki wa soka Tanzania waliojitokeza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jana walitoka vichwa chini baada ya timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites kufungwa mabao 4-0 na Zambia.
Kwa kipigo hicho, Tanzanites ni kama imekwishatolewa katika mbio za kuwania tiketi ya fainali za Afrika, kwani sasa inatakiwa kushinda 5-0 ugenini.
Ilikuwa huzuni kwa Watanzania wote waliojitokeza Uwanja wa Azam, Chamazi wakiongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi namna ambavyo Tanzanites walivyonyanyaswa na mabinti wenzao shupavu wa Zambia.
Tanzanites inayofundishwa na mzalendo, Rogasian Kaijage ilizidiwa kabisa na Shepolopolo Uwanja wa Azam na kujikuta hadi mapumziko ikiwa tayari imekwishabugizwa 3-0.
Mabao ya Shepolopolo yalifungwa na Memory Phiri dakika ya nne, Irene Lungu dakika ya 20 na Barbara Banda dakika ya 33.
Kipindi cha pili, Zambia walirudi na moto wao tena na kufanikiwa kupata bao la nne, mapema tu dakika ya 50 kwa penalti kupitia kwa Marry Wilombe.
Refa Batouli Ibrahim wa Sudan alitoa penalti hiyo baada ya Anastazia Anthony kumfanyia faulo mshambuliaj wa Zambia, Memory Phiri.
Wachezaji wa U20 ya wanawake ya Tanzania walionekana kabisa kuzidiwa na wenzao wa Zambia kwa kila kitu, nguvu, ufundi na hata maarifa.
Pamoja na madai ya kwamba, Zambia walitumia wachezaji wanane wa timu yao ya wakubwa- lakini haiondoi ukweli kwamba timu yetu ilikuwa dhaifu jana.
Na kuzidiwa huko ni matokeo ya maandalizi mabovu- tena mabovu kabisa.
Timu hiyo ilianza kuweka kambi katika hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Lakini ikiwa hapo, ilikosa fursa ya kutekeleza vizuri programu zake za mazoezi kwanza, kocha wa timu hiyo wakati huo huo alikuwa pia akiinoa timu ya wakubwa ya wanawake, Twiga Stars inayojiandaa na Michezo ya Afrika baadaye mwaka huu mjini Brazzaville, Kongo.
Lakini pia walijikuta wanashindwa kuutumia Uwanja wa Karume watakavyo- kwa sababu pia ulikuwa unatumiwa na klabu ya Yanga SC.
Kwa hivyo maandalizi ya timu mbili za taifa za wanawake yalikua ya ovyo ovyo- muda wote wa kambi ya Karume.
Wiki mbili kabla ya mchezo na Zambia, timu ikahamia Mbade, kuweka kambi katika nyumba ya kulala wageni ya Serengeti ambayo kwa mbele ina baa na ‘mziki mnene’.
Hiyo ndiyo baa na gesti kubwa na nzuri zaidi eneo la Mbade ambayo inavutia wakazi wengi wa eneo hilo. Hapo ndipo ilipowekwa timu ya taifa kujiandaa na mchezo waliofungwa 4-0 jana, ustaajabu nini kwa kipigo hicho?
Changamoto nyingine waliyokutana nayo Twiga ni kwamba Uwanja waliokuwa wanafanyia mazoezi, Azam Complex, pia walikosa fursa ya kuutumia watakavyo- kwa sababu wenyewe, Azam FC walikuwa wanautumia pia.
Mambo matatu haya; timu kukosa fursa nzuri ya kufanya mazoezi kwa sababu kila Uwanja waliopelekwa kulikuwa kuna timu inautumia, kocha wao kuwa na majukumu mengine pia Twiga Stars na kuwekwa kwenye kambi isiyostahii kule Mbade- kabisa yamechangia kipigo cha jana. Ramadhani Karim.

0 comments:
Post a Comment