KLABU ya Real Madrid imemuongezea Mkataba beki wa kushoto Mbrazil, Marcelo kwa miaka miwili zaidi, vigogo hao wa Hispani wametangaza jana.
Hatua hiyo itamfanya Marcelo awe mfanyakazi wa Uwanja wa Bernabeu hadi mwaka 2020.
Taarifa ya Real Madrid imesema: "Real Madrid imetangaza kuongeza Mkataba na Marcelo hadi Juni 30, 2020, kwa misimu mitano ijayo,".
Marcelo akipeana mikono na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez (kulia)
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Real kwa dau la Euro Milioni 6 kutoka Fluminense ya Brazil Januari mwaka 2007 na ni mchezaji wa tatu kwa umri mkubwa katika klabu hiyo nyuma ya Nahodha Iker Casillas na Nahodha Msaidizi Sergio Ramos.
Casillas anahusishwa na kuhamia Porto FC ya Ureno wakati Ramos anahusishwa na kuhamia Manchester United ya England- maana yake Marcelo anaweza kupewa beji ya Unahodha wa timu.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil ameichezea jumla ya mechi 320 klabu ya Real katika miaka yake tisa ya kuwa Madrid.
0 comments:
Post a Comment