KLABU ya Real Madrid ya Hispania ndiyo yenye themani kubwa zaidi katika michezo, mbele ya wababe wa NFL, Dallas Cowboys na MLB, New York Yankees kwa mwaka wa tatu mfululizo wajiwa waaongoza kwenye listi ya mwaka ya jarida la Forbes.
Washindi hao mara 10 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wanaongoza orodha ya jarida hilo wakiwazidi kwa zaidi ya Pauni Milioni 50 wapinzani wao wa La Liga, Barcelona wenye thamani ya Pauni Milioni 2,087.
Manchester United ndiyo klabu pekee ya Ligi Kuu England iliyoingia katika 10 Bora, wakifuatiwa na Manchester City, Chelsea na Arsenal katika orodha ndefu ya 50 Bora duniani.
Real Madrid ndiyo timu yenye thamani kubwa zaidi katika michezo kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes kwa mwaka wa tatu mfululizo
Jarida hilo la biashara la Amerika, Forbes limekuwa likitathmini timu katika michezo mikubwa na ligi mbalimbali tangu mwaka 1998, na timu kutoka nchini mwao, Marekani zimetawala kwenye orodha huku kwenye soka klabu saba tu zimeingia.
Nyuma ya Barca, wenye thamani ya Pauni Milioni 2,023 katika nafasi ya nne, kuna Man United, wenye thamani ya Pauni Milioni 1,975 kwenye nafasi ya tano, Los Angeles Lakers, New England Patriots, New York Knicks, Los Angeles Dodgers na Washington Redskins wanakamilisha 10 Bora.
Mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich wako nje ya 10 Bora wakiwa na thamani ya Pauni Milioni 1,502. Manchester City wapo nafasi ya 29, Chelsea nafasi ya 30 na Arsenal wapo nafasi ya 36.
Cha kufurahisha zaidi, timu za tatu zilizo juu kutoka Ulaya bara zinamilikiwa na wanachama, wakati timu za England zilizomo 50 Bora zote zinamilikiwa na watu binafsi.
Manchester United wana thamani ya Pauni Milioni 1,985 na ndiyo klabu pekee ya Ligi Kuu ya England katika 10 Bora, huku nyingine zikiishia 50 Bora.
0 comments:
Post a Comment